LANDESA

Ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) ambalo linashirikiana na serikali au taasisi mbalimbali katika kutetea na kulinda haki ya umiliki wa ardhi. Shirika hili limeweza kushirikiana na Sheria Kiganjani katika miradi ifuatayo:-.

MIRADI

LINDA ARHI YA MWANAMKE

Ni kampeni ya kimataifa ya kutetea na kulinda haki za ardhi ya mwanamke inayotekelezwa katika nchi mbalimbali duniani, kama vile Tanzania, Kenya, India, Liberia, Kolombia n.k. Kampeni hii imeratibiwa na mashirika ya kimataifa ikiwemo Hairou Commission, Habitat for Humanity, Benki ya Dunia, Landesa na mengine pia. Tanzania ndiye sekretariti wa kampeni hii, ambapo zaidi ya taasisi au asasi za kiraia 25 za kitanzania ni sehemu ya kampeni hii, inayotekelezwa sanjali na Malengo ya Maendeleo Endelevu yaani SDGs au Agenda ya 2030.

Landesa na Sheria Kiganjani waliingia mkataba katika kampeni hii mwaka 2019, kwa lengo la kulinda na kutetea haki za ardhi za wanawake haswa maeneo yenye uwekezaji mkubwa wa ardhi, pia kuongeza ushiriki thabiti wa wanawake katika vyombo vya maamuzi yanayohusu ardhi.

MWANAMKE NA ARDHI DATA COLLECTION TOOL

Mnamo mwaka 2019 mradi huu ulizinduliwa, ambapo LANDESA, Sheria Kiganjani na taasisi nyingine zilikuwa ni sehemu ya mradi. Mradi huu ulizinduliwa kwa lengo la kuwasaidia wasaidizi wa kisheria (Paralegals) katika wilaya ya Kimanzichana, mkoa wa Pwani, kuweza kukusanya taarifa, malalamiko au kesi kupitia njia au mfumo wa kidigitali maarufu kama Data Collection Tool.

Mfumo huo ulitengenezwa na Sheria Kiganjani, ambao unao uwezo wa kufanya kazi mahali ambapo hamna mtandao (offline) na baadae mtumiaji atakapokuwa mahali penye mtandao ataweza kutuma taarifa zote alizozirekodi.

Ambapo hadi kufikia mwisho wa mwaka 2020, zaidi ya wahudumu thelathini (30) wanatumia mfumo huo na kwa pamoja tulifanikiwa kukusanya jumla ya taarifa za watu 945.

COVID 19 EMERGENCY RESPONSE

Mbali na hapo, Sheria Kiganjani ilishirikiana tena na Landesa katika mradi wa miezi sita (6), yaani kuanzia mwezi wa nne hadi mwezi wa tisa mwaka 2020, katika kampeni ya kusambaza ujumbe kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID 19) uliopatiwa jina la COVID 19 Emergency Response. Mradi huu ulidhaminiwa na taasisi ya Bertha Foundation.

Mradi huu pia ulilenga kutetea haki na maslahi ya ardhi ya mwanawake aliyeajiriwa/kujiajiri au yule asiye na kazi yaani mama wa nyumbani. Hii ni kutokana na ongezeko kubwa la kesi za unyanyasaji wa kijinsia katika umiliki au utumiaji wa ardhi kwa mwanamke haswa katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Timu Yetu