i. Kumtaka mtu anayemtia nguvuni ajitambulishe kwajina, cheo, sehemu anayofanyia kazi na sababu zakumkamata,
ii. Kutumia lugha inayofahamika kwa mtuhumiwakatika kueleza sababu za kutiwa kwake nguvuni.
iii. Kutoteswa, kupigwa au kufanyiwa unyanyasaji waaina yeyote wakati akiwa mikononi mwa polisi aumtu aliyemkamata wakati ametii amri.
iv. Kupewa nafasi ya kutoa taarifa kwa mwanasheriawake, ndugu au jamaa zake kuhusiana na kutiwakwake nguvuni.
v. Kutonyang’anywa mali zake halali wakati wakutiwa nguvuni au baada ya kutiwa nguvuni.
vi. Kupatiwa matibabu kama ni mgonjwa au ameumiawakati wa zoezi la ukamataji.
vii. Kupatiwa dhamana toka kwa polisi kablahajafikishwa mahakamani kwa makosayanayodhaminika.
viii. Kukaa kimya.