i. Jamhuri ina dhamana na wajibu wa kuhifadhi nakulinda raia na mali zao dhidi ya wahalifu.
ii. Baadhi ya makosa ya jinai hayana madhara ya mojakwa moja kwa mtu binafsi na hivyo kukosekanakwa mtu ambaye ana nia na yuko tayari kufunguamashitaka dhidi ya mtuhumiwa.
iii. Makosa ya jinai hujumuisha adhabu ikiwa ni pamoja na mifungo.
iv. Makosa ya jinai yanahitaji gharama kubwa kwa mfano; kuchunguza, kuendesha mashitaka na kutunza watuhumiwa na baadae wafungwa.