-Ndugu wa marehemu na wale wenye maslahi na mirathi ya marehemu, kwa mfano wale ambao wanatarajia kupata sehemu ya mirathi ya marehemu. -Mtu au watu wanaomdai marehemu, mtu huyu hufungua mirathi pale ambapo ndugu wa marehemu wameshindwa au hawataki kufungua mirathi. -Kabidhi wasii mkuu. -Muwakilishi wa kisheria au mtu aliyetajwa kama msimamizi wa mirathi kwenye wosia. -Mtu yeyote ambaye mahakama kwa kuangalia vigezo mbalimbali vikiwamo undugu,maslahi ya muhusika katika mirathi hiyo, usalama wa mali za mirathi pamoja na uwezekano wa kusimamia vizuri, anaweza kuteuliwa na mahakama.