Mahakama yaweza kubatilisha uthibitishwaji wa mtekelezaji mirathi endapo itabaini yafuatayo;
• Kwamba mwenendo wa kupata utekelezaji au usimamizi wa mirathi ulikuwa na dosari za msingi.
• Kwamba utekelezaji au usimamizi wa mirathi ulipatikana kwa udanganyifu baada ya kutoa mapendekezo ya uwongo au baada ya kuificha mahakama habari muhimu na za msingi katika mirathi hiyo.
• Kwamba utekelezaji au usimamizi wa mirathi ulipatikana kwa njia ya malalamiko ya uwongo juu ya jambo la muhimu la kisheria ili kuthibitisha kupatikana kwa utekelezaji au usimamizi wa mirathi, ingawa malalamiko hayo yalifanywa kwa kutojua au bila nia mbaya.
• Kwamba utekelezaji au usimamizi wa mirathi umekuwa hauna maana na haitekelezeki.
• Kwamba mtu aliyepewa utekelezaji au usimamizi wa mirathi, kwa makusudi ameamua kutopeleka orodha ya mali za marehemu au amepeleka mahakamani orodha au taarifa ya uwongo ya mgawanyo wa mali za marehemu.