Wosia unaweza kuhifadhiwa ama kutunzwa mahali popote palipo na usalama na ulinzi ili kuepuka kughushiwa mfano; • Ofisi ya kabidhi wasii mkuu (RITA) • Kwenye vyombo vya kutoa msaada wa kisheria • Asasi za kidini kama kanisani au msikiti • Katika kampuni ya uwakili • Kwa mtu yeyote asiye mrithi katika wosia husika • Benki • Mahakamani, n.k.