Muusia anaweza kumnyima mrithi sehemu ya urithi wake ikiwa mrithi; -Amezini na mke wa muusia. -Amejaribu kumuua, amemshambulia au amemdhuru vibaya muusia au mama mzazi wa mrithi. -Bila sababu ya haki, hakumtunza muusia kutokana na njaa au ugonjwa. -Ameharibu mali ya muusia. Uharibifu huo utahesabika katika kukadiria kiwango cha urithi atakachostahili kupata.