Wosia wa maandishi ni lazima uzingatie yafuatayo; -Uandikwe kwa kalamu ya wino usiofutika kwa rahisi. -Anayetoa wosia lazima awe na akili timamu. -Wosia utaje tarehe ulipoandikwa. -Wosia utaje kuwa anayetoa wosia anafanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe. -Wosia ushuhudiwe na mashahidi wawili wanaojua kusoma na kuandika. Shahidi mmoja awe wa ukoo na mwingine awe mtu baki kama muusia anajua kusoma na kuandika. -Wosia hushuhudiwa na mashahidi wasiopungua wanne, mashahidi wawili wawe wa ukoo na wawili wawe watu baki kama muusia hajui kusoma na kuandika. -Wanaotarajia kurithi hawaruhusiwi kushuhudia wosia huo. -Wosia utiwe na saini ya muusia mbele ya mashahidi wake au kama hajui kusoma na kuandika aweke alama ya dole gumba la kulia. -Wosia utiwe saini na mashahidi.