Wajibu wa Msimamizi wa mirathi unajumuisha mambo yafuatayo: -Kufungua shauri la maombi ya usimamizi wa mirathi. -Kuainisha na kutambua mali na madeni yaliyoachwa na na marehemu. -Kulipa na kukusanya madeni yalioachwa na marehemu. -Kugawanya mali kwa warithi kulingana na sheria husika. -Kuwasilisha mahakamani hati inayoorodhesha mali na jinsi zilivyogawanywa katika mahakama ambapo shauri lilifunguliwa.