Hatua zifuatazo zitapaswa kufuatwa katika mazingira ambapo marehemu ameacha wosia:
• Taarifa ya kifo ikaandikishwe kwa Msajili wa vizazi na vifo katika muda wa siku 30.
• Kama wosia umemtaja mtu atakayekuwa msimamizi wa mirathi, msimamizi huyo afungue mirathi mahakamani akiwa na wosia ulioachwa, pamoja na cheti cha kifo.
• Ikiwa hakuna mtu aliyetajwa kuwa msimamizi wa mirathi, utaratibu wa wanandugu kukaa kikao ufanyike kumteua mtu atakayekuwa msimamizi wa mirathi.
• Mahakama hutoa tangazo la mirathi kwa muda wa siku 90 na kama hakuna pingamizi lolote, msimamizi hukabidhiwa barua ya kuhalalisha kugawa urithi na kulipa madeni.
• Baada ya ugawaji wa mali, msimamizi hupaswa kupeleka taarifa za ugawaji wa mali mahakamani na mahakama hufunga jalada baada ya kujiridhisha kwamba msimaizi wa mirathi ametekeleza majukumu yake kwa uaminifu na kwa mujibu wa Sheria.