Mgawanyo wa mali kwa sheria ya kiislamu huzingatia mambo yafuatayo; -Sharti ithibitike kwamba mwenye mali ameshafariki (maut-al-muwarith) -Kuwepo na warithi halali wa marehemu, yaani watoto wa marehemu na ndugu wengine na wote wawe warithi hakika wanaotambulika kisheria wakati wa mauti ya marehemu. (hayat-al-warith) -Marehemu awe ameacha mali -Urithi utokane na mali halisi na halali za marehemu.