Kwa mujibu wa kifungu namba 62 (I) (i) na (ii) cha sheria ya watu wenye ulemavu, adhabu zitolewazo kwa mtu/taasisi itakayo vunja matakwa ya sheria ya watu wenye ulemavu ni kama ifuatavyo, -Kwa taasisi ni faini isiyopungua milioni mbili na isiyozidi milioni ishirini -Kwa mtu binafsi faini isiyopungua laki tano na isiyozidi milioni saba au kifungo cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.