kifungu cha 42 Sheria ya Kazi na Mahusiano ya Kazi Namba 6 ya mwaka 2004, kinaeleza kama ifuatavyo; a) Kama mkataba wa ajira umekatishwa na mwajiri kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu ama ukiukwaji wa miiko ya kazi, basi mwajiri halazimiki kulipa kiinua mgongo. b) Kama mkataba wa ajira umekatishwa kutokana na mahitaji mapya ya uendeshaji wa ofisi/kazi ama kutokana na uanzishwaji wa teknolojia mpya inayohitaji watu wenye utaalamu zaidi, na mwajiri ametoa ajira mbadala kwa watakaoathirika na mabadiliko hayo, lakini wafanyakazi wakaikataa hiyo ajira mbadala basi mwajiri anaweza kukataa kulipa kiinua mgongo. c) Ni lazima mwajiriwa awe amehudumia katika ajira hiyo kwa muda usiopungua miezi 12 mfululizo ndipo atakidhi kigezo cha kupata kiinua mgongo. Aidha, lazima ukatishwaji huo wa mkataba uwe umesababishwa na mwajiri