Kifungu cha 33(1) cha sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini inamtaka mfanyakazi mwanamke atoe notisi kwa mwajiri kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, na notisi hiyo italazimika kuambatana na cheti cha kitabibu. Mfanyakazi anaweza kuanza likizo ya uzazi muda wowote kutoka wiki nne kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, au tarehe ya mapema kama tabibu atathibitisha kwamba ni muhimu kwa afya ya mfanyakazi au ya mtoto wake ambaye hajazaliwa