Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini inatoa maelekezo maalum juu ya watoto. Kwa mujibu wa sheria hii: a) Ni marufuku kwa mtu yeyote kumwajiri mtoto aliye na umri chini ya miaka 14. b) Mtoto aliye na umri wa miaka 14 anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi ambazo haziwezi kudhuru afya yake au kumzuia asiende shule au kuhudhuria mafunzo mbalimbali ya ufundi ambayo yana faida kwake c) Mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 haruhusiwi kuajiriwa kufanya kazi katika migodi, viwanda, meli na sehemu nyingine zozote ambazo kazi zake ni hatarishi.