Questions & Answers

Kodi ya mapato ni nini?

Hi ni kodi inayo katwa kwenye mapato ya mtu binafsi au chombo kama vile kampuni ambayo nayo ni mtu kisheria. Mfano wa mapato hayo ni kama vile; mshahara kutokana na ajira, faida katika biashara, gawio kutokana na uwekezaji n.k.

Kodi ya mapato ya shirika ni nini?

hii ni kodi inayolipishwa kwa faida inayoweza kutozwa kodi ya shirika kwa makampuni yote yaliyosajiliwa/ yanafanya shughuli za kibiashara nchini Tanzania.

Ushuru wa stempu ni nini?

hii ni kodi/ushuru maalumu unaotozwa kwenye bidhaa za filamu na muziki. Kwa Tanzania ushuru huu ulianza tangu mwaka 2012. Sheria inataka bidhaa zote ziwe za kuingizwa kutoka nje, au za kutengenezwa hapa ndani, kubandikwa stempu za kodi zinazosimamiwa chini ya sheria ya ushuru wa bidhaa.

kulipa kodi kwa njia ya kawaida ni kupi?

hii ni njia ambayo mlipa kodi anatumia kulipia kodi kwa kwenda ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania moja kwa moja au kituo kilicho karibu na kutekeleza jukumu la kulipa kodi.

Mahakama ya kodi ni nini?

hiki ni chombo maalumu ambacho kipo kisheria, ambacho kazi yaye kuu ni kusikiliza na kuamua mashauri yote ya kodi, kati ya wakusanya kodi na walipa kodi.

Mfumo wa makisio ya kodi ni nini?

huu ni mfumo wa kodi ambapo watu binafsi wasiokuwa na uwezo wa kutunza na kutengeneza hesabu za biashara hutozwa kodi kulingana na makisio ya mauzo ya mwaka. Na mlipa kodi alie katika mfumo huu hatakiwi na sheria za kodi ya mapato kuandaa na kutuma hesabu za ukaguzi mamlaka ya mapato (TRA).

Nini kazi ya mamlaka ya mapato?

kazi yake kubwa ni kuratibu shughuli zote za ukusanyaji mapato ya Serikali kuu, na kuratibu wakusanya kodi ambao wanafanya kazi chini ya chombo hicho.

Kodi ya majengo ni nini?

Kodi ya majengo ni tozo kwa mujibu wa sheria kwenye majengo/nyumba ambazo zimekamilika.

Je, kodi ya zuio kwa ajira ni nini?

kodi ya zuio mara nyingine huitwa kodi ya kukatalia, ni hitaji la serikali kwa mlipaji kwa kitu ki nacholeta mapato ili kukatalia au kupunguza kodi kutoka kwa malipo, na alipe kodi hiyo kwa serikali. Mfano wa kodi ya zuio ni kodi ya mshahara/mapato ya mfanyakazi.

Je, mashauri ya kodi huchukua mda gani hadi kuisha?

kuna kikomo cha mda lakini mara nyingi mashauri ya kodi yakiwa katika mahakama za kodi kwa ajili ya kuamuliwa huchukua miaka isiyopungua mitano na siyo zaidi ya mitatu kwa mujibu wa sheria.

Je, bidhaa kutoka nchi moja ya jumuiya ya Afrika Mashariki zinalipishwa kodi?

kwa lugha ya kigeni inaitwa (custom/import duty), hii ni kodi inayosimamiwa kwa mujibu wa sheria ya jumuiya ya Afrika Mashariki, wakazi wa jumuiya hiyo hawapaswi kulipa ushuru wa bidhaa kwa bidhaa zote zinazozalishwa na/au kusafirishwa ndani ya mipaka ya jumuiya.

Je, mamlaka ya mapato inaongozwa na nani?

Mamlaka ya mapato inaongozwa na kamishna mkuu wa mapato Tanzania, ambae kwa mujibu wa sheria huteuliwa na Rais ili kusimamia na kuratibu shughuli zote za ukusanyaji kodi na kuhakikisha kuwa sheria za kodi hazivunjwi.

Namba hiyo hutumika wapi?

namba hiyo hutumika kwa mawasiliano kati ya mlipa kodi na mamlaka ya mapato (TRA), katika maswala ya ardhi, leseni ya biashara na viwanda, usajili wa kampuni na mikataba yote ikihusisha ugavi wa bidhaa na huduma.

JE, kuna ulazima wa kuwasilisha hesabu za stempu za kodi?

ndiyo ni wajibu wa mwombaji kuwasilisha hesabu za matumizi ya stempu za kodi kila mwezi. Atawasilisha muhtasari wa ulinganisho wa hesabu za kila mwezi wa matumizi ya stempu zilizotolewa katika mwezi huo na zile zilizohamishwa kutoka miezi iliyopita.

Kwanini mashauri ya kodi husikilizwa tofauti na kesi zingine za kawaida?

yanasikilizwa kwa upekee kwani yanahitaji umakini wa hali ya juu sana, kwani yanahusisha mapato ya nchi, na kiujumla yamebeba maslahi mapana ya jamii na taifa kwa ujumla.

Je, kuna aina ngapi za kodi?

: kuna kodi inayolipwa moja kwa moja, na kodi inayo lipwa kupitia kwenye bidhaa yaani, kodi ya nyongeza ya thamani.

Je, chombo hiki kipo chini ya wizara gani?

chombo hiki kipo chini ya wizara ya fedha ambayo kazi yake kubwa ni kutunga sera na miswada mbali mbali ya sheria za kodi.

Je, kuna nini endapo mlipa kodi ya ardhi akakwepa kulipia au akachelewa?

Endapo ukachelewa kulipia kodi ya ardhi, baada ya tarehe 31, Desemba ya kila mwaka kisheria kodi hiyo mlipa kodi atailipa vikiambatana na tozo la adhabu.

Rufaa za kodi ni nini?

haya ni malalamiko ya mtu alie shindwa kulidhika na maamuzi ya mahakama ya kodi, hivyo kuamua kukata rufaa.

kodi/ushuru wa bidhaa ni nini?

hii ni kodi ambayo hutozwa kwenye bidhaa maalumu ambazo zinastahiki kutozwa, na inafanyika hivyo ili kulinda viwanda vya ndani na kulinda Tanzania isiwe sehemu ya kutupa bidhaa zilizopitwa na wakati ambazo hazifikii viwango vya ubora.

Je, ushuru/kodi ya kukuza ujuzi ni nini?

hii ni kodi ambayo mara nyingi hulipwa na waajiri ambao wanaajiri zaidi wafanyakazi wake, hutozwa kwa asilimia sita kutoka kwenye mishahara, pia asilimia mbili ya hiyo kodi huenda kwenye mamlaka ya elimu ya mafunzo ya ufundi kwa malengo ya kutoa ujuzi kwa wafanyakazi ambao waajiri wanahitaji.

kodi ya zuio ni nini?

hii ni kodi inayo kusanywa badala ya kodi ya mapato wakati wa kutoa huduma. Hii ipo ili kuhakikisha kuwa watu wanaostahili kulipa kodi ambao inawezekana kuwa vigumu kuwapata wanalipa kodi.

Kodi ya mauzo ya rasilimali ni nini?

hii ni kodi inayo lipwa mara moja kutokana na kuuza mali au kitega uchumi.

Kodi chini ya mfumo wa makisio ya kodi ni ipi?

hii ni kodi inayo lipwa na mlipa kodi na inatokana na mauzo ya mwaka ya mlipa kodi kama yalivyo tathminiwa na kamishina wa kodi ya mapato.

Kodi inayolipwa na wasafirishaji ni ipi?

hii ni kodi inayolipiwa na watu wenye vyombo vya usafirishaji wa abiria, na hulipwa kila kituo ambapo chombo hicho hupita wakati wa kusafirisha abiria.

Nini maana ya kodi ya biashara za kimataifa?

hii ni kodi inayolipwa na makampuni au wafanya biashara wanaofanya biashara kutoka nchi moja kwenda nyingine inajumuisha ushuru wa forodha, kodi ya bidhaa, kodi ya nyongeza ya thamani kwenye bidhaa n.k.

Utozwaji wa kodi kwa watu wenye mapato ya kawaida ni nini?

hii ni kodi inayolipwa na wafanyabiashara binafsi wadogo waliochini ya mfumo wa makisio ambao hawana uwezo wa kutunza kumbukumbu za biashara zao au zile za wafanya biashara wanao tunza kumbukumbu za biashara zao.

Mashauri ya kodi ni nini?

hii ni migogoro kati ya walipa kodi na wakusanya kodi, au mgogoro kati ya mlipa kodi na mamlaka ya mapato Tanzania.

Namba ya utambulisho ya mlipa kodi ni nini?

Hii ni namba maalumu inayotolewa na mamlaka ya mapato (TRA) kwenda kwa mlipa kodi, namba hiyo hutolewa kwa mtu mmoja tu. Kwa lugha ya kitaalamu huitwa (TIN) Taxpayer Identification Number.

Majukumu ya Mahakama ya rufaa ya kodi ni yapi?

hiki ni chombo ambacho kipo kusikiliza malalamiko ya mtu yeyote ambaye hajalidhika na maamuzi ya mahakama ya kodi.

Mamlaka ya mapato ni nini?

Hiki ni chombo cha serikali maalumu kinacho fanya kazi chini ya wizara ya fedha, kazi yake kubwa na kusimamia na kuratibu shughuli zote za ukusanyaji wa kodi Tanzania.

Je, mamlaka ya mapato ni nini?

Hiki ni chombo maalumu ambacho kimeanzishwa chini ya sheria ya mamlaka ya mapato Tanzania, sheria iliyo tungwa na Bunge.

Je, kanuni za kodi ni nini?

hizi taratibu au misingi inayo wasaidia watunga sheria ili kuweza kutunga sheria nzuri za kodi, kutengeneza mifumo mizuri ya yakodi na kadhalika

Stempu za kodi kielektroniki ni nini?

Huu ni mfumo maalumu ambao umeanzishwa na serikali katika kuimarisha usimamizi wa kodi ndani ya nchi. Wanufaikaji wa mfumo huu ni Serikali, wazalishaji, na watumiaji ambapo faida yake kubwa ni kulinda mapato ya Serikali kwa kuzuia bidhaa bandia.

Ushuru wa forodha ni nini?

huu ni ushuru unaotozwa kwenye bidhaa zinatoka au kuingia inchini kupitia mamlaka zenye dhamana katika maeneo husika.

Je, kuna masharti yeyote mtu kuweza kupata stempu za kodi?

ili kuweza kupata stempu za kodi mtu yeyote kwanza ni lazima atimize masharti ambayo ni kama vile; lazima awe amesajiliwa na kupatiwa idhini na mamlaka ya kutoa leseni, aombe kupatiwa stempu za kodi, ambatanisha nyaraka zinazoonesha kuwa bidhaa ni ya mwombaji n.k.

Nani anakusanya kodi?

Inayo kusanya kodi ni serikali kupitia mamlaka iliyokwa na serikali, yaani mamlaka ya mapato ya Tanzania.

Kodi zinazokusanywa na serikali za mitaa husimamiwa na nani?

kama ambavyo tumeona katika serikali kuu kuwa kodi hizo zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, hivyo basi katika serikali za mitaa mara nyingi ukusanyaji kodi unasimamiwa na halmashauri za wilaya katika maeneo husika na kuhakikisha zinafanya malengo yaliyo kusudiwa.

Je, kuna nafuu yeyote mashahidi wanapewa(posho)?

kama ambavyo tumeona kwamba mashauri haya yanabeba maslahi mapana ya jamii na taifa kwa ujumla, hivyo kwa mujibu wa sheria mashahidi wanapewa posho katika kipindi chote cha kusikiliza mashauri ya kodi.

Kwanini sheria za kodi hubadilika kila wakati?

kama hali ya uchumi inavyo badilika kila wakati hata sheria za kodi kama ambavyo ni sheria zinazotumika kusimamia uchumi, nazo hubadilika ili kuendana na hali ya uchumi, lakini pia zinabadilika kutokana na mwaka wa fedha wa serikali.

kivipi kodi inaporomosha uchumi?

kama tulivyo sema mwanzoni kuwa kodi inakuza uchumi lakini hiyo hiyo kodi inaporomosha uchumi, hasa pale kodi inapowekwa na mamlaka husika bila kuangalia hali ya uchumi ya walipa kodi, kodi ikiwa kubwa sana walipa kodi wengi watashindwa kulipa kodi na hatimae serikali itakosa fedha ya kuweza kuendeshea miradi ya kimaendeleo na hatimae kushuka kwa uchumi.

Je, mashahidi wanaruhusiwa mahakama za kodi?

kama yalivyo mashauri mengine na mahakama inahitaji kupata ushahidi wa kutosha ili kuweza kuamua mashauri pasina shaka na kuhakikisha kila mtu ameridhika na uamuzi.

Nini maana ya mwaka wa mapato?

katika muktadha wa kodi ya mapato, mwaka wa mapato una maana ya kalenda ya mwaka wa miezi 12, lakini linapokuja swala la makampuni inaweza kuomba kwa maandishi kwa kamishna kibali cha kubadili mwaka wake wa mapato kutoka mwaka unaoanza januari kwenda mwaka unaoanzia wakati mwingine unaopendekezwa na asasi/kampuni.

Kumbukumbu gani muhimu zinahitajika wakati wa malipo?

Kisheria kwa wale ambao kumbukumbu zao za umiliki wa ardhi tayali zilisha ingizwa kwenye kompyuta wanatakiwa wakumbuke namba ya kumbukumbu ya kulipia yenye tarakimu sita, au wengine wanatakiwa kuwa na risiti/stakabadhi ya mwisho ya malipo na nakala ya hati au barua ya toleo.

Kodi halali ni ipi?

Kodi halali ni ile inayo kusanywa na serikali kwa mujibu wa sheria, pia ni kodi iliyo tajwa na sheria halali ya kodi iliyo tungwa na Bunge.

Je, kuna uhusiano wowote kati ya kodi na haki za binadamu?

kodi halali ni ile wakati wa ukusanyaji wake inazingatia haki za binadamu na sio kuvunja haki za binadamu, mfano haki ya kufanya kazi. Na haki zingine zote zilizopo kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria zingine za kimataifa zinazo husika na haki za binadamu.

Kivipi kodi inakuza uchumi?

kodi inakuza uchumi kwa kuongeza zaidi vyanzo vya uchumi, au inakuza uchumi kwa kuongeza thamani ya fedha pale kunapokuwa na fedha nyingi mtaani, serikali huweka kodi kubwa hasa kwenye bidhaa ili kufanya makusanyo kuwa mengi na hatimae kukuza uchumi. Nchi nyingi Duniani uchumi wao unakuwa kwa kutumia kodi.

Je, kodi ya ardhi hulipwa wakati gani?

kodi ya ardhi hulipwa mwaka wa fedha wa Serikali unaoanza tarehe 1 mwezi wa saba kila mwaka.

Kodi ya ardhi ni nini?

kodi ya ardhi ni malipo ya pango la ardhi wanayotozwa wamiliki wa viwanja na mashamba yaliyopimwa na kumilikishwa kisheria.

Je, kodi zote ni lazima kulipia?

kodi ya lazima kulipia ni ile iliyopo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizo tungwa na Bunge au Mamlaka ya mapato Tanzania, lakini zamani kulikuwa na kodi ya kichwa ambayo kwa Tanzania tangu tumepata uhuru kodi hiyo haipo tena, na kodi zingine kama hizo.

Nini maana ya kodi ya makampuni?

kodi ya makampuni ni kodi inayotozwa katika mapato yanayotozwa kodi ya asasi kama vile makampuni yenye dhima ya ukomo na makampuni mengine ikiwa ni pamoja na vilabu,vyama,jumuiya na vikundi vingine visivyo shiriki.

Kodi ya ongezeko la thamani ni nini?

kodi ya ongezeko la thamani ni kodi ya matumizi ya moja kwa moja au si ya moja kwa moja. Inatumika kwa miamala yote ya bidhaa na huduma katika mnyororo wa uzalishaji na usambazaji hadi hatimae bidhaa inapokuwa imetumika.

Je, kodi zote zimetajwa kwenye sheria za Bunge?

kodi zote lazima zitajwe kwenye sheria iliyo tungwa na Bunge, lakini kuna kodi zipo kwa sheria zilizotungwa na serikali za mitaa au halmashauli katika eneo husika.

Je, nani anapanga kiwango cha kodi?

kodi zote zinapagwa na mamlaka ya mapato ya Tanzania na sheria zilizo tungwa na Bunge, au Serikali za mitaa katika maeneo yao pia na Halmashauri za wilaya.

Je, unaweza kukusanya kodi bila sheria?

Kodi zote zipo kwa mujibu wa sheria, na kukusanya kodi bila sheria huo ni wizi kwani, katiba ya nchi imetamka kuwa kodi zote lazima ziwepo kwa mujibu wa sheria.

Je kuna majengo yasiyo tozwa kodi ya majengo?

kuna majengo yasiyo tozwa kodi ya majengo, mfano kibanda cha udongo, nyumba ya nyasi na , makuti, na zingine zinazo fanana nazo.

Nini vya kuzingatia wakati wa kupanga viwango vya kodi?

kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kupanga viwango vya kodi, lakini kabisa cha muhimu ni idadi ya walipa kodi walio sajiliwa, hali ya kiuchumi ya walipa kodi, kanuni na taratibu za kodi, na vyanzo vya mapato katika eneo husika.

Endapo kuna mgogoro kati ya mlipa kodi na mkusanya kodi, nani anashughulika na utatuzi huo?

kuna mtu anaeteuliwa na serikali yeye kazi yake ni kuhakikisha sheria za kodi zinafuatwa lakini pia kama kuna mgogoro kati ya mlipa kodi na mkusanya kodi basi huo mgogoro utafikishwa kwake kwa utatuzi zaidi, kwa lugha ya kitaalamu anaitwa (tax ombudsman service)

Je, njia gani hutumika kukadiria kodi ya majengo?

kuna njia ambazo zimekuwa mahususi Tanzania kwenye kukadiria kodi za majengo mfano njia ya simu ya mkononi ambapo mmiliki atawasiliana na mamlaka husika au njia ya tovuti ya mamlaka ya mapato Tanzania.

Je, kuna athari zozote endapo makadirio ya kodi yakafanyika nje ya maeneo tajwa hapo juu?.

kuna uwezekano wa makadirio kutokuwa sahihi, kuna uwezekano wa kuwepo kwa lengo la kughushi ambalo ni kosa la jinai kisheria, kupoteza fedha zako wewe mlipa kodi, ukipatikana na nyaraka za kughushi utashitakiwa kwenye vyombo vya dola na kupata usumbufu ambao unaweza kuepukika.

Je, kwanini kipindi cha nyuma wajasiliamali wengi walipunguziwa kodi hadi kufikia elfu ishirini?

lengo kubwa la Serikali ya kipindi hicho ilikuwa ni kufanya wajasiliamali mitaji yao ikue na hatimae kupanua wigo wa walipa kodi, ni kama ambavyo tumeona sasa hivi Mh. Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ameamua kusema nae kwamba watu wanao anza biashara hasa wenye mitaji midogo wasilipe kodi kwa mwaka mmoja, lengo ni kutaka mitaji yao ikue na hatimae serikali iweze kukusanya kikubwa hapo baadae kutoka kwa wafanya biashara hao.

Makadirio na malipo ya kodi ya ardhi yanafanyika wapi?

Makadirio hufanywa kwenye ofisi za ardhi zinazotambulika za Manispaa na Halmashauri za Miji na Wilaya.

;Je, mlipa kodi anahaki gani?

mlipa kodi ana haki ya kupewa taarifa kuhusu kodi anayo paswa kulipia, anahaki ya kuheshimiwa utu wake sio akishindwa kulipia adhalilishwe, kwani haki zote za mlipa kodi zipo kwa mujibu wa sheria.

Je, kwanini mlipa kodi apewe risiti?

Mlipa kodi ni lazima apewe risiti kwani inampa uhakika kuwa kodi inaenda sehemu husika pia inampa uhakika kuwa ameshiriki kwenye shughuli za maendeleo ya nchi yake.

Je, nini wajibu wa mlipa kodi?

mlipa kodi yeyote anawajibu wakulipa kodi, kwani kufanya hivyo ni kutii agizo la kikatiba na pia ni utekelezaji wa sheria zilizo tungwa na bunge za kodi.

Je, kuna uhusiano wowote kati ya kodi na demokrasia?

moja kati ya misingi ya demokrasia ni pamoja na uwazi,uwajibikaji, sasa basi kama wakusanya kodi watakuwa wawazi kwa kutoa taarifa za kodi zilizo kusanywa au pale wanapokiuka sheria wakawajibishwa basi kwa namna hiyo misingi ya demokrasia itakuwa imezingatiwa.

Nini maana ya motisha ya kodi?

Motisha ya kodi inatafsiriwa kama punguzo, kuachwa au msamaha wa kodi inayotakiwa kulipwa, inatolewa ili kuwa kama kivutio ili kuingiza katika shughuli maalum kama vile uwekezaji katika bidhaa mtaji kwa muda maalumu. Motisha ya kodi ni mfumo wa kifedha wa motisha ya uwekezaji inajumuisha likizo ya kodi ya mapato kwa mashirika makubwa na punguzo la kiwango cha kodi ya mapato.

Je, kuna adhabu yeyote kwa mtu anae kwepa kodi?

mtu yeyote mwenye wajibu wakulipa kodi akigundulika kuwa anakwepa kulipa kodi, basi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Kwani ni wajibu wa kila mtu alie fikisha umri wa miaka kumi na nane kulipa kodi kwani ni agizo la kisheria.

Nani anapaswa kulipia kodi ya ardhi?

Mtu, yeyote anayemiliki ardhi iliyopimwa kisheria iwe imeendelezwa au haijaendelezwa anapaswa kulipa kodi ya pango.

Je, kuna ulazima wa mlipa kodi kusajiliwa?

ndio ulazima upo ili serikali iweze kufahamu idadi ya walipa kodi, pia ili kuweza kurahisisha shughuli nzima ya kukusanya kodi.

Je, kuna athari yeyote endapo sheria za kodi zikashindwa kubadilishwa kwa mda mrefu?

ndiyo kuna athari endapo sheria zitashindwa kubadilishwa, kwani kodi zote zipo kwa mujibu wa sheria kwa hiyo kushindwa kubadilisha sheria kwa mda mrefu itafanya upotevu mkubwa sana wa mapato yanayo kusanywa kwani kutakuwa hakuna sheria inayosimamia ukusanyaji huo.

Je, kodi ya nyongeza ya thamani ni nini?

Ni kodi ya jumla ya matumizi kwenye nyongeza ya thamani ya bidhaa na huduma kwa kiwango cha kawaida cha asilimia kumi na nane. Ni kodi ya ambayo mara nyingi hutoka kwa mtumiaji wa mwisho wa bidhaa flani.

kwanini kodi ya ardhi inalipwa?

Ni kutimiza masharti/mkataba unaomtaka mmiliki kulipia kodi ya pango la ardhi kila mwaka, pia unalipa kodi ya ardhi kwa kunufaika na matumizi ya ardhi hiyo kwa kipindi ulichopewa.

Kodi ni nini?

Ni mchango wa lazima unaowekwa na serikali kwa wananchi, ili kukusanya mapato na kuweza kupata fedha ya kukidhi matumizi ya serikali.

Kwanini ukinunua kitu ni lazima udai risiti na ukiuza utoe risiti.

ni takwa la kisheria na kushindwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria pamoja na katiba ya nchi ambayo sheria za kodi hupata uhalali kutoka kwenye katiba.

Je, nani anafaa kulipa kodi?

Ni, mtu yeyote aliefikisha umri wa miaka kumi na nane na mwenye uwezo wa kulipa kodi, na anaepata huduma za serikali.

Je, serikali za mitaa zinakusanya kodi?

Serikali za mitaa kama ambavyo zimeanzishwa na katiba ya nchi, na kupewa mamlaka na sheria ya Bunge, zina mamlaka ya kukusanya kodi hasa katika maeneo yao.

Ni taarifa/rekodi gani zinazopaswa kuhifadhiwa na walipa kodi?

sheria ya kodi ya mapato inamtaka kila mtu binafsi anayepaswa kulipa kodi katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kutunza nyaraka zote ili kuwezesha uamuzi sahihi wa kodi inayolipwa.

Je vivutio vya kodi ni nini?

Sheria za kodi zinatoa misamaha mbali mbali kwa biashara za aina fulani ili kutoa vivutio vya uwekezaji. Misamaha mingine hutolewa kwa sababu za kisiasa au kijamii. Vivutio hivyo hutoa nafuu kwa kulipa kodi fulani, kwa kawaida kodi ya mapato, kodi ya zuio, kodi ya ongezeko la thamani(VAT) na ushuru wa forodha.

Je, ni halali mlipa kodi endapo akashindwa kulipa kodi mali zake kuchukuliwa au biashara yake kufungwa?

sio halali kwani kufanya hivyo ni kuvunja haki yake ya kumiliki mali na pia kuvunja haki yake ya kufanya kazi, kwani haki zote zipo kikatiba.

Je, stempu za kielektroniki zinahusisha bidhaa gani?

stempu za kielektronic zinatumika kwa bidhaa zilizoorodheshwa kwa mujibu wa sheria ambapo zinaweza kubadilika kutokana na maboresho yanayotokea. Mfano wa bidhaa hizo ni kama vile mvinyo, pombe kali, maji ya kunywa, sigara, bia, vilainishi, sharubati(juisi), bidhaa za manukato, bidhaa za filamu na muziki. 96.

Nini maana ya taarifa ya mapato ya kodi?

taarifa ya mapato ya kodi ni maelezo yanayowasilishwa mamlaka ya mapato Tanzania yanayoonesha makadirio ya mapato na kodi inayolipwa au mapato ya mwisho na kodi inayolipwa kwa kila mwaka wa mapato.

Kampuni ni nini?

Tafsiri ya neno kampuni inaweza kuwa na maana tofauti tofauti kutokana na mtu anavyo tafsiri. Lakini kwa lugha ya kawaida kampuni hizi ni asasi za kibiashara zinazo tambulika chini ya sheria ya makampuni Tanzania.

Kwanini tunalipa kodi?

Tunalipa kodi ili serikali iweze kupata mapato ya kuweza kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo, na huduma za kijamii.

Kwanini tunalipa kodi?

tunalipa kodi moja ili kuimarisha uchumi, ili serikali ipate fedha ya kufadhili miradi ya kimaendeleo, ili serikali ipate mapato ya kuweza kulipia matumizi yake n.k.

Je, kulipa kodi kwa njia ya simu ya mkononi ni halali?

ulipaji kodi kwa njia ya simu ni rahisi kwani hufanya kila mtu mwenye wajibu wa kulipa kodi kutekeleza jukumu hilo bila hata kwenda kwenye ofisi za kodi au mamlaka ya mapato.

JE, ushuru wa stempu za kodi unakokotolewaje?

ushuru wa stempu za kodi unakokotolewa kulingana na stempu za kodi zilizoombwa kwenye bidhaa za filamu na muziki katika mwezi husika na stempu ambazo hazijatumika katika mwezi huo katika ulinganisho wa mwezi hivyo kuchukuliwa kuwa zimepotea.

Je, wakati wa kupanga aina ya kodi ni vitu gani muhimu vya kuzingatia?

Vitu vya kuzingatia ni haki za binadamu, hali ya kipato ya mlipa kodi, sheria inasema nini kuhusu kodi hiyo na vitu vingine vinavyo husika.

Je, majengo yote hutozwa kodi kwa viwango sawa?

viwango vya malipo ya kodi ya majengo vinapangwa kwa kuzingatia aina ya nyumba na mahali jingo lilipo.

Je, wabia wanapaswa kulipa kodi ya makampuni?

wabia hawalazimiki kulipa kodi ya mapato. Hata hivyo wabia wanatozwa kodi ya mapato katika faida zinazosambazwa kutoka kwenye ubia kwa kuzingatia uwiano wa uchangiaji uliokubalika.

Je, wakusanya kodi wanapaswa kuzingatia nini wakati wa kukusanya kodi?

wakati wa kukusanya kodi kuna mambo mengi ya kuzingatia, kama vile hali ya mlipa kodi kifedha, usitumie nguvu sana, usichukue au kufunga biashara ya mlipa kodi pale anaposhindwa kulipia na kadhalika.

Je, wakusanya kodi wanawajibu gani?

wakusanya kodi kama watu walio aminiwa na serikali kwa niaba ya wananchi basi wanatakiwa kuhakikisha kodi zote zinazokusanywa zinaingizwa kwenye mfuko wa Taifa ili kuweza kutekeleza malengo yaliyo kusudiwa kupitia kodi hizo.

Je, wakusanya wanatoa wapi mamlaka?

wakusanya kodi wanapata mamlaka kutoka kwenye sheria za kodi, na sheria zingine za utumishi wa umma. Lakini kama hakuna sheria inayo wapa mamlaka wanafanya makosa na huo utakuwa ni wizi kama wizi mwingine.

Ni nani wanapaswa kulipa kodi ya makampuni?

wanaopaswa kulipa kodi ya makampuni ni makampuni yenyewe, yenye dhima ya ukomo,amana,klabu, makampuni ya ndani ya kudumu n.k.

Je, wigo wa kodi ni nini?

wigo wa kodi ni jumla ya idadi ya watu/vyombo vilivyo sajiliwa kama walipa kodi na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA). Hawa ni pamoja na waajiriwa, watu waliojiajiri na biashara pamoja na mashirika.

Je, Wizara ya fedha inamamlaka kwenye idara ya kodi?

Wizara ya fedha ina mamlaka kwenye idara ya kodi, kwani wizara ya fedha ndio inatunga sera mbali mbali za kodi, na kupendekeza kutungwa sheria mpya ya kodi mfano SERA YA TOZO.

Unaelewa nini kuhusu kodi na ushuru wa Biashara nchini Tanzania?

wizara ya fedha kama ilivyo na dhamana ya mapato nchini Tanzania, inawajibika kubainisha muundo na uainishaji wa kodi inayopaswa kulipwa kutoka kwenye maeneo mbali mbali ya kibiashara.

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand