Questions & Answers

Je ni upi utaratibu wa kuwasilisha lalamiko katika tume ya Upatanishi?

a) Mlalamikaji ajaze fomu maalum na nakala ya fomu hiyo atapewa mwajiri ambaye mlalamikaji anamlalamikia ili malalamikiwa au walalamikiwa wajibu madai dhidi yao. b) Tume itawaita wahusika wote.

Je ndani ya muda gani mwajiriwa anapaswa kuwasilisha lalamiko lake?

a) Muda wa kuwasilisha lalamiko lake tangu kuachishwa kazi utokee ni ndani ya siku 30. b) Migogoro mingine yoyote ya kikazi haina budi kuwasilishwa ndani ya siku 90 tangu ilipotokea.

Je, Tanzania kuna vyama gani vya wafanyakazi?

a) TUCTA: Shirikisho huru la vyama vya wafanyakazi-huu ni munganiko wa vyama vyote b) RAAWU: chama cha watafiti na waalamu wafanyakazi mbalimbali?. c) CWT: Chama cha Walimu Tanzania d) CHODAWU: Chama cha wafanyakazi wa mahotelini, mshambani na majumbani (please cross-check) e) TUICO: Chama cha wafanyakazi wa viwandani na taasisi za fedha f) JT: Chama cha waandishi wa Habari g) TAMICO: Chama Cha wafanyakazi wa Migodi na Ujenzi (please cross-check) h) TALGWU: Chama Cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa i) TUGHE: Chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na Afya (kindly cross-check)

Majukumu ya vyama vya wafanyakazi ni yapi?

a)Kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi wote bila kuwabagua kwa misingi ya kijinsia, rangi,imani,itikadi na hadhi b) Kutetea upatikanaji wa hali bora za kazi c) Kushughulikia utatuzi wa migogoro ya kikazi. d) Kuwakilisha wanachama katika ngazi zote za kitaifa na za kimataifa e) Kuelimisha wafanyakazi kuhusu haki zao.

Je, baada ya kuachishwa kazi, mfanyakazi ana stahiki zipi?

Baada ya kusitisha ajira, mwajiri anapaswa kumlipa mfanyakazi malipo yafuatayo; a) Malipo kwa kazi yote aliyoifanya kabla ya kuachishwa kazi, na ambayo haijalipiwa. b) Likizo yoyote ambayo ni stahili ya mwajiriwa, ambayo haijachukuliwa. c) Mshahara wa mwezi mmoja badala ya notisi, kama mwajiri attamua kusitisha mkataba mara moja. d) Nauli ya mfanyakazi, wategemezi na mizigo yake kwenda mahali ambako alikuwa anaishi kabla ya kuajiriwa kwa mujibu wa kumbukumbu alizoandikisha wakati wa kuajiriwa e) Malipo mengine stahiki kwa mujibu wa sheria, kama vile malipo ya hifadhi ya jamii, kiinua mgongo, nk kulingana na makubaliano ya mkataba.

Je ni vigezo vipi utumika katika kutoa stahiki baada ya kuachishwa kazi?

Baadhi ya stahiki hizi zinatolewa kulingana na vigezo mbalimbali kama: a) Sababu ya kukatishwa mkataba b) Aina ya mkataba wa ajira c) Muda ambao mwajiriwa amehudumu katika ajira

Je ni lazima kwa mwajiri kutoa hati ya kazi (Certificate of Service)?

Hii ni hati anayopatiwa mwajiriwa anayeacha/anayeachishwa kazi kutambua mchango wa nguvukazi yake katika huduma/kazi ambayo amekuwa akiifanya katika muda wote wa ajira yake katika kampuni/taasisi husika. Hati ya kazi haitakiwi kueleza sababu za kuacha/kuachishwa kazi

Je mwajiriwa ana haki zipi baada ya mkataba kuisha ama kukatishwa?

Hizi ni stahiki azipatazo mwajiriwa kutokana na mkataba wake wa ajira kukatishwa na mwajiri. Stahiki hizi hulipwa na mwajiri. kipengele cha 44 cha Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004 inampa mwajiriwa haki ya kulipwa stahiki mbalimbali pindi mkataba wake wa kazi unapokatishwa.

Je mwajiriwa mwanaume anastahili likizo ya uzazi?

Ikiwa mfanyakazi ni mwanaume na mke wake amejifungua mtoto basi mfanyakazi huyo mwanaume anayo haki ya kupata likizo ya uzazi ya siku 3 . Likizo inapaswa ichukuliwe ndani ya siku 7 tangu mtoto kuzaliwa.

Wakati mwingine makampuni ya kibishara hufilisika na kufungwa. Ikitokea hivyo, ni upi utaratibu wa kuachisha wafanyakazi?

Iwapo utatokea usitishaji wowote wa ajira ya wafanyakazi kwa sababu zaza kiuendeshaji, mwajiri atatakiwa kufuta utaratibu ufuatao; a) Kutoa notisi ya kusudio la kupunguza wafanyakazi mapema iwezekanayo b) Kutoa taarifa zote muhimu zinazohusiana na upunguzaji wa wafanyakazi uliokusudiwa kwa ajili ya mashauriano mazuri. c) Kushauriana na chama cha wafanyakazi kabla ya kupunguza wafanyakazi

Je, notisi ya kuachishwa kazi inapaswa kutolewa wakati gani kwa mfanyakazi?

Kama mkataba wa ajira unaweza kusitishwa kwa notisi, muda wa notisi hautakuwa pungufu ya; a) Siku 7, kama notisi inatolewa katika mwezi wa kwanza wa ajira b) Siku 4 kama mfanyakazi ameajiriwa kwa msingi wa kulipwa kwa siku au wiki. c) Siku 28 kama mfanyakazi ameajiriwa kwa msingi wa kulipwa kwa mwezi.

Je Katiba ya nchi inalinda haki ya kuajiriwa?

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inalinda haki za kiuchumi. Haki za kiuchumi ni pamoja na haki ya kufanya kazi na usawa katika sehemu za kazi. Haki hii imeainishwa katika ibara ya 22 ya Katiba. Na Ibara ya 23 imetoa haki ya kupata ujira na malipo ya haki kulingana na kazi ambayo mtu ameifanya.

Je ni nini kitapaswa kufanyika iwapo mwajiriwa haelewi kilichoandikwa katika Mkataba wa Ajira?

Kifungu cha 15(3) kimeweka wazi kuwa kama mfanyakazi haelewi maelezo yaliyoandikwa , mwajiri atapaswa kuhakikisha kwamba maelezo yaliyomo katika mkataba yanafafanuliwa kwa mfanyakazi kwa kiwango ambacho kitamwezesha mfanyakazi kuelewa.

Je mwajiri anaweza kubadili mkataba wa ajira bila kumhusisha mfanyakazi?

Kifungu cha 15(4) kinaelekeza bayana pale ambapo suala lililotajwa katika kifungu kidogo cha 15(1) litabadilika, mwajiri atatakiwa kwa kuwasiliana na mfanyakazi, kurekebisha maelezo yaliyoandikwa ili kuendana na mabadiliko na kumtaarifu mfanyakazi mabadiliko hayo kwa maandishi. REBUILD PLEASE

Je, likizo ya uzazi huombwaje?

Kifungu cha 33(1) cha sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini inamtaka mfanyakazi mwanamke atoe notisi kwa mwajiri kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, na notisi hiyo italazimika kuambatana na cheti cha kitabibu. Mfanyakazi anaweza kuanza likizo ya uzazi muda wowote kutoka wiki nne kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, au tarehe ya mapema kama tabibu atathibitisha kwamba ni muhimu kwa afya ya mfanyakazi au ya mtoto wake ambaye hajazaliwa

Je ni ipi tafsiri ya kiinua mgongo

kifungu cha 42 Sheria ya Kazi na Mahusiano ya Kazi Namba 6 ya mwaka 2004, kinaeleza kama ifuatavyo; a) Kama mkataba wa ajira umekatishwa na mwajiri kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu ama ukiukwaji wa miiko ya kazi, basi mwajiri halazimiki kulipa kiinua mgongo. b) Kama mkataba wa ajira umekatishwa kutokana na mahitaji mapya ya uendeshaji wa ofisi/kazi ama kutokana na uanzishwaji wa teknolojia mpya inayohitaji watu wenye utaalamu zaidi, na mwajiri ametoa ajira mbadala kwa watakaoathirika na mabadiliko hayo, lakini wafanyakazi wakaikataa hiyo ajira mbadala basi mwajiri anaweza kukataa kulipa kiinua mgongo. c) Ni lazima mwajiriwa awe amehudumia katika ajira hiyo kwa muda usiopungua miezi 12 mfululizo ndipo atakidhi kigezo cha kupata kiinua mgongo. Aidha, lazima ukatishwaji huo wa mkataba uwe umesababishwa na mwajiri

Je sheria inazuia vipi ubaguzi katika kupata ajira?

Kifungu cha 7 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kinaharamisha ubaguzi wa aina yoyote kwenye masuala ya ajira na mahali pa kazi, ikiwemo ubaguzi wa moja kwa moja na ule usio wa moja kwa moja kwa mfano: a) Ubaguzi wa rangi b) Kabila c) Dini d) Kisiasa e) Jinsi f) Jinsia g) Ubaguzi kutokana na ujauzito h) Hali ya ulemavu

Nini maana ya kuachishwa kazi isivyo halali?

Kuachishwa kazi isivyo halali ni pale ambapo mwajiri atashindwa kuthibitisha uhalali wa kumuachisha kazi mfanyakazi, au kutokuwa na sababu za msingi zinazoendana na matendo, utendaji na/au uwezo wa mfanyakazi, na hujumuisha pia kushindwa kuthibitisha kuwa kuachishwa kazi kwa mfanyakazi kulikuwa sahihi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Je ni kwa muda gani mwajiri anatakiwa kutunza mkataba wa ajira?

Kwa mujibu wa kifungu cha 15 (5) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini mwajiri anapaswa kutunza Mkataba kwa muda wa angalau miaka mitano baada ya ajira kukoma

Je mkataba wa ajira wa maandishi unatakiwa kuwa na vipengele gani?

Kwa mujibu wa kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi, maelezo ya mkataba kwa maandishi yanayojumuisha:- i. Jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi ii. Mahali alipoajiriwa iii. Kazi yake iv. Tarehe ya kuanza v. Muundo na muda wa mkataba vi. Kituo cha kazi vii. Masaa ya kazi viii. Ujira, njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine au malipo ya vitu (Sampuli ya Mkataba wa Ajira inapatikana katika tovuti ya www.sheriakiganjani.co.tz)

Je ajira ni nini?

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (taja kifungu ikiwezekana), ajira ni kitendo cha mtu kufanya kazi katika shirika, kampuni au kwa mtu binafsi kwa makubaliano ya kulipwa ujira maalum.

Je ni mahakama zipi zenye kusikiliza migogoro ya kazi?

Kwa mujibu wa sheria ya Taasisi za Kikazi, utatuzi wa migogoro ya ajira inashughulikiwa na vyombo vifuatavyo:- a) Tume ya Upatanishi na usuluhishi b) Mahakama kuu ya Tanzania (kitengo cha kazi) c) Mahakam ya Rufani.

Je ni muda gani mwajiriwa baada ya kujifungua anapaswa kurudi kazini?

Mfanyakazi aliyejifungua atapaswa kurudi kazini wiki zisizo pungua 6 tangu ajifungue, isipokuwa kama daktari anayetambulika ameelekeza vinginevyo.

Baada ya muda wa likizo kuisha, mama anapaswa kuendelea kunyonyesha. Je ni masaa mangapi katika siku moja ambayo mfanyakazi anaruhusiwa kuyatumia kwa kunyonyesha?

Mfanyakazi ana haki ya masaa hadi mawili kwa siku ya kumnyonyesha mtoto wakati wa saa za kazi. Mgawanyo wa masaa wawili utategemea na makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa.

Je likizo ya uzazi hutolewa kwa siku ngapi?

Mfanyakazi anastahili likizo ya uzazi kama ifuatavyo:- a) Siku 84 za likizo ya uzazi yenye malipo iwapo amejifungua mtoto mmoja. b) Siku 100 za likizo ya uzazi yenye malipo iwapo amejifungua watoto mapacha c) Siku 84 za ziada za likizo ya uzazi yenye malipo ndani ya mzunguko wa likizo yake, iwapo mtoto wake atafariki ndani ya mwaka mmoja wa kuzaliwa na mfanyakazi huyo atapata ujauzito na kujifungua kabla ya miezi 36 kupita

Je mwajiriwa yupi ana stahili kupewa likizo ya mwaka?

Mfanyakazi anayestahili likizo ni yule ambaye tayari ameshafanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja. Kwa mwajiriwa wa msimu (kipindi kifupi)ikiwa amefanya kazi kwa mwajiri huyo huyo kwa zaidi ya mara moja kwa mwaka na ikiwa vipindi hivyo alivyofanya kazi vinazidi miezi 6 na kundelea katika mwaka huo, basi anastahili likizo yenye malipo.

Je ni utaratibu gani unatumika katika kutoa malipo ya likizo ya ugonjwa?

Mfanyakazi atawasilisha cheti cha daktari kuthibitisha ugonjwa wake, na mwajiri hatapaswa kumlipa mwajiriwa likizo ya ugonjwa endapo mwajiriwa atashindwa kuwasilisha cheti cha daktari.

Je ni sababu zipi haziwezi kutumika kumwachisha mfanyakazi kazi?

Mfanyakazi hawezi kuachishwa kazi kwa sababu zifuatazo; a) kufukuzwa kazi kwa sababu zinazohusiana na ujauzito,kufanya hivyo ni kujunja sheria b) kuachishwa kazi kwa sababu zinazohusiana na ulemavu c) kuachishwa kazi kwa sababu zinazohusiana na ubaguzi mfano kwa sababu ya jinsia yake,dini yake, itikadi yake kisiasa,kabila lake. d) ikiwa mfanyakazi atafichua taarifa ambazo mfanyakazi ana haki au anatakiwa kufichua kwa mtu mwingine kwa mujibu wa sheria. e) Kama mfanyakazi amejiunga au slijiunga kwenye chama chochote cha wafanyakazi

Nini maana ya mikataba isiyokuwa na muda maalum?

Mkataba usiokuwa na muda maalum ni mkataba ambao ukomo wa ajira haujatajwa waziwazi. Chini ya mkataba huu mfanyakazi anaweza kuendelea na kazi mpaka kufikia umri wa kustaafu endapo haitatokea sababu yoyote ya kusitisha ajira kabla ya umri huo wa kustaafu.

Nini maana ya mkataba wa Muda Maalum?

Mkataba usiokuwa na muda maalum ni mkataba ambao ukomo wa ajira haujatajwa waziwazi. Chini ya mkataba huu mfanyakazi anaweza kuendelea na kazi mpaka kufikia umri wa kustaafu endapo haitatokea sababu yoyote ya kusitisha ajira kabla ya umri huo wa kustaafu.

Nini maana ya mkataba wa Kazi Maalum?

Mkataba wa kazi maalum ni aina nyingine ya mkataba wa muda maalum ambao hutegemea kumalizika kwa kazi na malipo hufanyika kwa siku au baada ya kumalizika kwa kazi husika.

Je likizo ya mwaka kwa mwajiriwa inapaswa kuwa ya siku ngapi?

Mwajiriwa anastahili kupata likizo ya siku 28 kwa mwaka. Likizo hii haiathiri mshahara wake. katika pindi hiki cha likizo, siku zote zitahesabiwa, zikiwemo zile za mapumziko ya mwisho wa wiki na sikukuu.

Je Likizo ya ugonjwa inatolewa kwa muda gani?

Mwajiriwa anastahili likizo ya ugonjwa ya siku 126. Likizo hii imegawanyika katika mafungu mawili -Siku 63 za kwanza za likizo ya ugonjwa, ambazo zitakuwa na malipo kamili ya mshahara. -Siku 63 za pili za likizo ya ugonjwa, ambazo zitakuwa na malipo ya nusu mshahara.

Je kuna aina nyingine ya likizo?

Ndiyo, mfanyakazi ana angalau siku 4 za likizo, isiyoathiri mshahara wake, kwa sababu zifuatazo: -Ugonjwa au kifo cha mtoto wa mfanyakazi -Kifo cha mke wa mfanyakazi, mzazi, bibi au babu, mjukuu au kitukuu

Je, mwajiri anawajibika kuzuia ubaguzi mahali pa kazi?

Ndiyo. Kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Mwajiri analazimika kusajili kwa Kamishna wa Kazi, mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi, Kamishna wa Kazi anaweza kumtaka mwajiri a) Kuunda mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi kama inavyoelekezwa katika kifungu kidogo cha (2); na b) Kuusajili mpango huo kwa Kamishna Kutokuunda mpango huo na kuusajili ni kosa kisheria

Je kuna faida za kujiunga na vyama vya wafanyakazi?

Ndiyo. Ni nyingi. Miongoni mwa hizo ni: a) Kupata uwakilishi pindi unapotokea mgogoro wa kimaslahi kazini baina ya mwajiri na mfanyakazi. b) Kutetea haki za wafanyakazi zisipindishwe na mwajiri , kwa mfano; haki ya likizo, mafao bora, nk c) Kwa niaba ya wafanyakazi, kuhamasisha waajiri kuweka mazingira bora, salama na yenye staha kazini. d) Kuwaelimisha wanachama wao juu ya haki zao za kazi, na namna bora ya kuzidai haki hizo.

Je, upo wakati ambao haufai notisi ya kusitisha ajira kutolewa?

Ndiyo. Notisi ya kusitisha ajira haitakiwi kutolewa Wakati wa kipindi cha likizo yoyote ya kazi kwa mujibu wa sheria (mfano likizo ya mwaka, likizo ya uzazi, kufiwa, nk)

Nini maana ya vyama vya wafanyakazi?

Ni taasisi zinazoanzishwa kisheria na wafanyakazi ili kuwaunganisha waweze kutetea haki zao na maslahi yao kazini kwa sauti moja. Inajumuisha pia kupigania mafao bora kulingana na uzalishaji wao kazini. Maslahi ya wafanyakazi yanajumisha pia mazingira bora na yenye staha ya kufanyia kazi.

Je notisi ya kusitisha ajira inatakiwa iweje?

Notisi ya kusitisha ajira itakuwa kwenye maandishi, ikieleza sababu ya kusitisha na tarehe ambayo notisi inatolewa.

Je, jukumu la kuthibitisha kwamba kuachishwa kazi kwa mfanyakazi kulikuwa halali ni la nani?

Pale ambapo mahakama inahitaji kujiridhisha ili kulitolea maamuzi shauri lililoko mbele yake, ni jukumu la Mwajiri kuthibitisha kwamba sababu za kumwachisha kazi mwajiriwa/mfanyakazi, na utaratibu uliofuatwa ni sahihi na haki

Kuna aina ngapi za mikataba ya ajira?

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini imeigawa mikataba ya ajira katika aina kuu tatu ambazo ni; a) Mkataba isiyokuwa na muda maalum b) Mkataba wa muda maalum c) Mkataba wa kazi maalum

Je ni upi muda stahili wa mwajiriwa kufanya kazi?

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini imeweka kiwango cha juu cha kufanya kazi kama ifuatavyo; a) Siku 6 kwa wiki b) Saa 45 kwa wiki c) Saa 9 kwa siku

Je mtoto anaweza kuajiriwa?

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini inatoa maelekezo maalum juu ya watoto. Kwa mujibu wa sheria hii: a) Ni marufuku kwa mtu yeyote kumwajiri mtoto aliye na umri chini ya miaka 14. b) Mtoto aliye na umri wa miaka 14 anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi ambazo haziwezi kudhuru afya yake au kumzuia asiende shule au kuhudhuria mafunzo mbalimbali ya ufundi ambayo yana faida kwake c) Mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 haruhusiwi kuajiriwa kufanya kazi katika migodi, viwanda, meli na sehemu nyingine zozote ambazo kazi zake ni hatarishi.

Je, mfanyakazi ana haki ya kisheria ya kujiunga na vyama vya wafanyakazi? Au anaweza kufanya hivyo kwa hisani tu ya mwajiri?

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, na Sheria ya Taasisi ya za kazi zinatoa haki kwa wafanyakazi wote kuanzisha na kujiunga na vyama vya wafanyakazi na kwa waajiri kuunda vyama vya waajiri. Kwa hiyo, haki ya kujiunga na chama cha wafanyakazi au chama cha waajiri inalindwa kwa mujibu wa sheria

Je mwajiriwa ana stahili aina ngapi za likizo?

Sheria ya Ajira na Mahusiano kAZINI2004, na sheria ya Taasisi za kazi 2004 zimetoa aina za likizo mbalimbali kama vile; a) Likizo ya mwaka b) Likizo ya ugonjwa c) Likizo ya uzazi d) Likizo ya ulezi

Je ni vigezo vipi huufanya mkataba kuwa halali?

Uhalali wa mkataba ni lazima ujengwe katika nguzo kuu tano ambazo ni: a) Makubaliano b) hiari ya kuingia mkataba c) malipo halali d) sifa/vigezo vya kuweza kuingia katika mkataba e) uhalali wa shughuli yenyewe itakayofanyika

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand