Questions & Answers

Je, ni adhabu gani ambazo hutolewa kwa makosa ya jinai?

-Adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, uhaini na kusababisha mgomo katika jeshi la wananchi. -Kulipa Faini -Kulipa Fidia -Kifungo cha Gerezani au cha nje -Kuchapwa Viboko -Kutaifisha au kunyang`anya mali -Kuwa chini ya matazamio ya kutotenda kosa ndani ya muda maalum -Kuwa chini ya Afisa Ustawi kwa kufanya shughuli za mafunzo maalum -Kutumikia jamii

Utetezi wa ugonjwa wa akili utakubalika katika mazingira gani?

-Alikuwa haelewi analolifanya wakati anatenda kosala jinai. -Alishindwa kujitambua au kutambua kwamba -Hakupaswa kufanya yale aliyofanya. -Hakuwa na uwezo wa kuzuia au kudhibiti kosalisifanyike.

Utetezi wa kutenda kosa kwa msukumo wa ulevi unakubalika katika mazingira gani?

-Hali ya ulevi imetokea bila ridhaa ya mtuhumiwatoka kwa mtu mwingine ambaye amemlewesha kwa hila na ulaghai. -Kutokana na kuleweshwa akili za mtuhumiwaziliathirika kiasi cha kutojitambua au kutotambuaalilolifanya wakati anatenda kosa la jinai.

Japokuwa, mahakama ina uwezo wa kukataa kutoa dhamana katika shitaka lolote lile kukiwa na mazingira yafuatayo:

-itathibitika kwamba mtuhumiwa amewahikutumikia kifungo kinachozidi miaka mitatu. -itathibitika kwamba mtuhumiwa amewahi kupewadhamana lakini akakiuka masharti ya dhamana hiyo. -mahakama itaona kwamba ni vema mtuhumiwaasipewe dhamana kwa sababu.

Vitu gani vinapaswa kuwepo kwenye hati ya mashtaka?

-Iwe imetolewa na Mkuu wa Kituo cha polisi,hakimu au mtendaji. -Lazima iwe na mhuri wa polisi, mahakama aumtendaji. -Iwe imesainiwa -Lazima iwe na maelezo ya mtuhumiwa kama vile jina, -Ielezee tuhuma na sababu za kukamatwa nakufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma

Ni sababu gani ambazo zinafanya Jamhuri kuendesha kesi za jinai?

-Jamhuri ina dhamana na wajibu wa kuhifadhi nakulinda raia na mali zao dhidi ya wahalifu. -Baadhi ya makosa ya jinai hayana madhara ya mojakwa moja kwa mtu binafsi na hivyo kukosekanakwa mtu ambaye ana nia na yuko tayari kufunguamashitaka dhidi ya mtuhumiwa. -Makosa ya jinai hujumuisha adhabu ikiwa ni pamoja na mifungo. -Makosa ya jinai yanahitaji gharama kubwa kwa mfano; kuchunguza, kuendesha mashitaka na kutunza watuhumiwa na baadae wafungwa.

Je, ni haki zipi za msingi ambazo raia au mtuhumiwa anazo katika mfumo wa makosa ya jinai?

-kila mtuhumiwa ana haki ya kuthaminiwa utu naheshima yake au kutoteswa pale anapotiwa nguvuni -kila mtuhumiwa ana haki ya kuelezwa kosaalilotenda kabla ya kukamatwa. -kila mtuhumiwa ana haki ya kupewa ushauri wakisheria. -Ana haki ya matibabu pale anapokuwa ameumizwaau anaumwa. -Ana haki ya chakula na malazi. -Ana haki ya kuwasiliana na ndugu zake. -kila mtuhumiwa ana haki ya kukaa kimya mpakapale anapo hitaji huduma ya kuwakilishwa. -kila mtuhumiwa ana haki ya kupata dhamanaisipokuwa kwa makosa yasiyokuwa na dhamana. -kila mtuhumiwa ana haki ya kuyafahamu mashitakayake. -kila mtuhumiwa anahesabiwa kuwa hana hatia hadihapo chombo chenye mamlaka (mahakama) yakuzisikiliza tuhuma kitakapomsikiliza na kumuonana hatia dhidi ya kosa analotuhumiwa. -Kila mtuhumuwa atachukuliwa kuwa mwenye akilitimamu katika sheria ya makosa ya jinai hadi hapoitakapothibitishwa vinginevyo mbele ya sheria.

Je, ni nini mamlaka ya polisi katika mfumo mzima wa jinai Tanzania?

-kulinda amani na utulivu katika nchi -kuwatia nguvuni na kuwaweka watuhumiwa chiniya kizuizi (mahabusi) -kuwafikisha watuhumiwa mahakamani -kupepeleza mashauri ya watuhumiwa -kutoa ushahidi mbele ya mahakama dhidi yawatuhumiwa wa makosa ya jinai -kusaidia katika majanga ya kitaifa.

Ni haki gani ambazo mtuhumiwa anazo wakati wa kukamatwa?

-Kumtaka mtu anayemtia nguvuni ajitambulishe kwajina, cheo, sehemu anayofanyia kazi na sababu zakumkamata. -Kutumia lugha inayofahamika kwa mtuhumiwakatika kueleza sababu za kutiwa kwake nguvuni. -Kutoteswa, kupigwa au kufanyiwa unyanyasaji waaina yeyote wakati akiwa mikononi mwa polisi aumtu aliyemkamata wakati ametii amri. -Kupewa nafasi ya kutoa taarifa kwa mwanasheriawake, ndugu au jamaa zake kuhusiana na kutiwakwake nguvuni. -Kutonyang`anywa mali zake halali wakati wakutiwa nguvuni au baada ya kutiwa nguvuni. -Kupatiwa matibabu kama ni mgonjwa au ameumiawakati wa zoezi la ukamataji. -Kupatiwa dhamana toka kwa polisi kablahajafikishwa mahakamani kwa makosayanayodhaminika. -Kukaa kimya.

Baada ya mahakama kusikiliza pande zote katika kesi, ni maamuzi gani yanaweza kutolewa?

-kumwachia huru mshitakiwa kwa kutokuwa na hatia, pale upande wa mashitaka unaposhindwa kuthibitisha mashitaka na utetezi wa mshitakiwa kukanusha mashitaka hayo. -kumtia hatiani mtuhumiwa na kumhukumu kutumikia adhabu, kama upande wa mashitaka utathibitisha mashitaka dhidi ya mshitakiwa pasipo shaka yoyote na utetezi wake kushindwa kukanusha mashitaka hayo.

Je, mtuhumiwa ana haki gani wakati wa mahojiano?

-Kupata utambulisho kutoka kwa askari polisianayefanya mahojiano. Hii ni pamoja na kuelezeajina, cheo chake na sababu za kutiwa nguvuni. -Kuelezwa kwa lugha fasaha inayoeleweka kwamtuhumiwa. -Kupata tahadhari kutoka kwa askari polisi anayehojikwamba hawajibiki kujibu maswali yote isipokuwayale yanayohusu maelezo binafsi (wasifu wake) najina lake. Hivyo mtuhumiwa ana haki ya kutojibu. -Kuwasiliana na mwanasheria wake au ndugu zakeakiwa mikononi mwa polisi, isipokuwa kama kunasababu ya msingi ya kuzuiliwa asiwasiliane na haowahusika. -Kuthaminiwa utu wake pamoja na haki zake zabinadamu. -Kupatiwa matibabu anapokuwa yu mgonjwa auamejeruhiwa katika hatua za ukamataji.

Je, ni masharti gani yanayoambatana ndhamana inayotolewa na mahakama?

-Kusalimisha hati ya kusafiriakwa polisi au vyombovingine husika. -Kumzuia mtuhumiwa kusafiri nje ya eneo maalumu. -Kumtaka mtuhumiwa kuripoti kwenye kituo chapolisi kwa muda maalumu. -Kumzuia mtuhumiwa asionekana au kutembeleamaeneo maalumu. -Masharti mengineyo ambayo mahakama itaonainafaa.

Ni wajibu gani ambao mtuhumiwa anao wakati wa kukamatwa?

-Kutii sheria pasipo shuruti; -Kutii amri halali ya polisi wakati anatiwa nguvuni. -Kujibu maswali atakayoulizwa na polisi au mtuyeyote anayemkamata. -Kutoa taarifa sahihi ambazo atatakiwa kutoa mbeleya askari polisi au mtu yoyote anayemkamatazinazohusiana na kutendeka kwa kosa la jinai aukushiriki kwake katika kosa la jinai. -Kutoa ushirikiano mbele ya polisi.

Upekuzi unatakiwa ufanywe kwa njia zipi?

-Kuwepona hati ya upekuzi. -Kufanyika kwa upekuzi bila hati ya upekuzipale ambapo sheria inatoa mwanya kutokana namazingira. Kwa mfano, mtuhumiwa kuaminikakuwa ana silaha au kitu chochote kinachohatarishausalama na amani kwa umma. -Kufanyika kwa upekuzi nyakati za mchana yaanikati ya jua kucha na kupwa (kati ya mawio namachweo). Hata hivyo upekuzi unaweza kufanyikamuda mwingine wowote kama mahakama imetoaidhini ya kufanya hivyo. -Kufanyika kwa upekuzi mbele ya mashahidi ambaowanaweza kuwa: kiongozi wa mtaa au shina au mtumzima yeyote mwenye akili timamu. -Kama itatokea kuna vitu au mali imechukuliwakwa ajili ya ushahidi, basi ni lazima iandikishwe namhusika au mwenye mali kutia sahihi kuthibitishakutwaliwa kwa mali hizo. -Kutunzwa katika sehemu salama vitu au malizilizochukuliwa kabla ya kurejeshwa kwa mmilikihalali.

Utawala wa haki jinai kwa ujumla umejikita katika kanuni kuu zifuatazo:-

-Lazima kuwepo na sheria inayoainisha kwa uwazi kwamba matendo flani yanapofanywa na watu kuwa ni jinai. -Sheria hiyo lazima pia ianishe adhabu kwa matendo hayo ambayo ni makosa ya jinai. -Wajibu wa kuthibitisha shitaka dhidi ya mshitakiwa ni wa yule anyelalamika, na kwa Tanzania ni Jamhuri, hivyo upande wa mashitaka unapaswa kuthibitisha shitaka lake dhidi ya mshitakiwa pasipo kuacha shaka. -Mtuhumiwa atachukuliwa kuwa hana hatia mpaka itakapodhibitika hivyo. -Mtu yoyote hatapelekwa gerezani pasipo kufikishwa kwanza Mahakamani.

Je ni mazingira yapi yanapelekea utetezi wa kughadhabishwa au Kukasirishwa kukubalika?

-maneno yaliyotamkwa au kitendo kilichofanywa si kosa la jinai na ni halali kisheria. -kosa la jinai lililofanywa linatokana na ushawishi, kusisimka na jazba ambazo zimetokana na mtu mwingine au matendo ya mtu mwingine. -itathibitika kwamba kitendo hicho hakikuwa halali na ni kinyume cha sheria.

Kabla mtu hajapata dhamana lazima atimize masharti ya dhamana ambayo ni pamoja na yafuatayo:

-Mdhamini wake au mtuhumiwa kusaini na kuingiamakubaliano na polisi au ofisi na Mkurugenzi wa Mashitaka, TAKUKURU au Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali kwamba atahudhuria mahakamanisiku anayotakiwa. -Mara baada ya kusaini au kuingia makubaliano hayona vyombo husika kama ilivyoelezwa hapo juu basimtuhumiwa atatoka kwa dhamana kama atakuwayuko gerezani au mahabusu.

Ni sababu zipi mahakama inaweza kuzitumia kumpunguzia mshtakiwa adhabu?

-Mshitakiwa kutenda kosa kwa mara ya kwanza -Mdhoofu waugonjwa ama umri mkubwa.

Ni mazingira yapi yatamfanya mtu au askari kumkamata mtuhumiwa bila kuwa na hati ya mashtaka?

-mtu atafanya tendo la kuvunja amani mbele yaaskari, -mtu atamzuia askari polisi kufanya kazi zake, auatafanya jaribio la kutoroka au atatoroka kutokachini ya ulinzi, -mtu ataonekana kuwa na mali ya wizi auinayoshukiwa kuwa ya wizi, -mzururaji au mtu anayezurura kwa nia ya kufanyauhalifu, -mtu anayehisiwa kuwa hati ya kukamatwaimeshatolewa dhidi yake, -mtu yeyote ambaye amefanya kosa nje ya Tanzaniana kuna uwezekano wa kuadhibiwa ndani yaTanzania, -mtu anayedharau nembo ya taifa kama vile wimbowa Taifa au Bendera ya Taifa

Je, ni nani anayeweza kupeleka mashtaka ya jinai?

-Mtu yeyote -Chombo cha dola. Mf. Polisi, TAKUKURU

Je, dhamana ya polisi inaweza kufutwa? Na ni katika mazingira yapi?

-Mtuhumiwa haonekani, yaani mtoro au; -Ameshindwa au anaelekea kushindwa kuzingatiamasharti ya dhamana.

Je, ni mambo gani yanatakiwa kuzingatiwa katika kutoa dhamana polisi?

-Mtuhumiwa kujidhamini kimaandishi aukuthibitisha kwa maandishi kwamba atafikamahakamani siku na muda uliopangwa. -Mtuhumiwa kuhakikisha kimaandishi kwambaatazingatia na kufuata masharti ya dhamanaatakapokuwa nje. -Mtu mwingine anayeaminika mbele ya askari polisianaweza kumdhamini mtuhumiwa. -Uwezo wa mtuhumiwa au mdhamini kulipa kiasicha fedha endapo mtuhumiwa atashindwa kufikamahakamani siku iliyopangwa kusikiliza shaurilake.

Upelelezi hulenga kujibu mambo yafuatayo;

-Tukio limetokea wapi -Limetokeaje -Limetokea wakati gani -Nani ni mhusika wa tukio hilo na kwa nini ametenda tukio hilo

Kinga hizo ni zifuatazo;

-Ugonjwa wa akili -Kutenda Kosa kwa Msukumo wa Ulevi -Umri Mdogo -Haki ya Kujilinda au Kujihami -Kulazimishwa au Kushurutishwa Kutenda Kosa la jinai -Kushitakiwa na Kuadhibiwa kwa Kosa Hilohilo -Kushitakiwa na Kuachiwa Huru -Mtuhumiwa Kutokuwepo Eneo la Tukio -Kughadhabishwa au Kukasirishwa -Kuchukua au Kufanya Kitendo Dhidi ya Mali Halali

Je, ni vigezo vipi hutumika katika kutoa dhamana?

-Uhakika wa mtuhumiwa kufika mahakamani sikuatakayotakiwa kufanya hivyo. Katika kujiridhishana kigezo hiki, askari polisi huzingatia yafuatayo; -Historia ya maisha ya mtuhumiwa na mahusianoyake na jamii au, ajira yake -hali ya familia yake, na -Kumbukumbu/rekodi au habari za maisha yaketoka kwa polisi. -Mazingira ya kosa au tuhuma. -Maslahi ya mtuhumiwa, yaani Kipindi atakapotakiwa kukaa mahabusu kamadhamana itakataliwa ikiwa ni pamoja namazingira ya mahabusu penyewe, -Mahitaji au haja ya mtuhumiwa kuwa nje kwalengo la kuandaa utetezi wake au kufika kwakemahakamani, ikiwa ni pamoja na kupata ushauriwa kisheria na uwakilishi mahakamani, -Mahitaji ya kiusalama ya mtuhumiwa ambayoyanaweza kutokana na ulevi wa kupindukia,majeraha au matumizi ya madawa ya kulevya, -Usalama wa jamii hasa uwezekano wa mtuhumiwakuharibu ushahidi kwa kuwatisha mashahidi aukuwazuia polisi kufanya upelelezi.

Je, ni taratibu gani zinatumika kumtia nguvuni mtuhumiwa?

-Ukamataji kwa Kutumia Hati ya mashataka. -Ukamataji bila Kuwa na Hati ya mashtaka.

Je, askari polisi anatakiwa kutoa au kutumia silaha katika kumkamata mtuhumiwa?

Askari polisi au mtu yeyote anayekamata mtuhumiwaharuhusiwi kutumia nguvu au na silaha dhidi ya mtuhumiwa Zaidi ya kuhakikisha kuwa hatoroki.

Je, ni sahihi kwa askari polisi kumsababishia maumivu makali au hata kifo mtuhumiwa wakati wa kumkamata?

Askari polisi haruhusiwi kufanya jambo loloteambalo linaweza kusababisha maumivu, majerahamakali na hata kifo kwa mtuhumiwa isipokuwa kamaitaonesha na yeye kuamini kwa dhati kwamba kwakufanya hivyo atakuwa amelinda na kuhifadhi maisha aukuzuia madhara makubwa kwa binadamu.

Nini kinatakiwa kifanyike baada ya kunakili mahojiano hayo katika maandishi?

Baada ya kunakiliwa katika maandishi, mtuhumiwa atasoma/atasomewa maelezo hayo ndipo asaini na afisa polisi asaini hati ya mahojiano baada ya mahojiano hayo.

Nini maana ya ombi la kupunguziwa adhabu na mahakama?

Baada ya mahakama kumtia hatiani mshitakiwa, nakabla ya mahakama kutoa adhabu hutoa mwanya wamaombi kwa pande zote ya ama kupunguza adhabu aukutoa adhabu kama ilivyo kwenye sheria.

Mshtakiwa anapaswa kufanya nini baada ya kusomewa mashtaka?

Baada ya shitaka kusomwambele ya mshitakiwa, mshitakiwa hupaswa kujibu kwaama kukiri kutenda kosa, au kukana kutenda kosa.

Dhamana inatolewa na nani?

Dhamana huwezakutolewa na -Jaji au Hakimu -Mkuu wa kituo cha Polisi.

Nini maana ya dhamana?

Dhamana ni ruhusa ya kuwa nje ya mahabusu au gereza anayopewa mtuhumiwa aumshitakiwa wakati akisubiri shitaka lake kupelekwa aukusikilizwa mahakamani au akisubiri hatma ya rufaayake.

Nini wajibu wa raia baada ya kumkamata mtuhumiwa?

Endapo mtuhumiwa atakamatwa na raia, basi ni wajibuwa raia kumfikisha mtuhumiwa mbele ya kituo cha polisiharaka iwezekanavyo.

Je, kukata rufaa au kuomba mrejesho ni haki ya mshtakiwa?

Haki ya kukata rafaa, kuomba marejeo au kuombamapitio ni haki ya kikatiba na kila mshitakiwaanastahili haki hiyo.

Je, mtuhumiwa akiomba dhamana polisi, anatakiwa kutoa pesa au mali yoyote?

Hapana, dhamana inayotolewa na jeshi la polisi haihusiani na kuweka dhamana mali au pesa zake.

Je, kila mtuhumiwa ana haki ya kupata dhamana?

Hapana, si kila mtuhumiwa ana haki ya kupata dhamana. Kuna baadhi ya makosa kama mauaji na uhaini ambayo mtu akishtakiwa nayo hapati haki ya dhamana.

Je, ni sahihi kwa askari polisi kumdhalilisha mtuhumiwa wakati wa kumkamata?

Hapana, si sahihi kwa askari polisi au mtu awaye yeyote kumdhalilisha mtuhumiwa Zaidi ya kuhakikisha kuwa mtuhumiwa hatoroki.

Je, haki hii ipo kwa upande wa mshatakiwa peke yake?

Hapana, Upande wowote usiporidhika na maamuzi ya mahakama unayo haki ya ama kuomba kurudia kwahukumu katika mahakama ileile; kukata rufaa au kuombamarejeo dhidi ya hukumu katika mahakama ya juu ya ileiliyotoa hukumu na yenye mamlaka ya kusikiliza rufaaau marejeo.

Je, ukamataji kwa kutumia hati nini?

Hati ya ukamataji ni hati inayotoa amri ya kukamatwa mtuhumiwa wa jinai. Hati hii inaweza kutolewa na vyombo mbali mbali ikiwamo polisi, mlinzi wa Amani (mtendaji wa kijiji au kata), hakimu na jaji.

Je, ni hatua zipi zinazochukuliwa katika hatua ya kukamatwa hadi kupata adhabu?

Hatua ya kukamatwa hadiadhabu hupitia hatua zifuatazo -Kukamatwa kwa Mtuhumiwa -Upelelezi wa Makosa ya Jinai -Upelekaji wa Mashauri ya Jinai Mahakamani -Uendeshaji Mashauri ya Jinai Mahakamani -Dhamana -Ushahidi Mahakamani -Hukumu itolewayo na Mahakama -Adhabu -Rufaa

Vipi ikitokea mtuhumiwa ni motto (umri chini ya miaka 18)?

Ikiwa mtuhumiwa anayehojiwa ni mtoto, afisa wa polisi mpelelezi (mfawidhi) anayemhoji mtoto huyo aliye chini ya uangalizi wa polisi, atawajibika kuwataarifu wazazi ama ndugu wa mtoto huyo kwamba, mtoto husika yupo kituo cha polisi kwa tuhuma ambazo ametuhumiwa nazo na yupo kwa mahojiano juu ya tuhuma hizo.

Je, ni nani anaendesha kesi za jinai?

Jamhuri ndio yenye dhamana kupitia waendesha mashtaka kuendesha kesi zote za jinai kwa niaba ya wananchi.

Kwa nchini Tanzania, ni chombo gani kilicho mstari wa mbele katika mfumo huu wa haki jinai?

Jeshi la Polisi kwa kiasi kikubwalinahusika katika maeneo ya ukamataji, uhifadhi wa watuhumiwa baada ya kukamatwa, mfumo wa kuwahoji watuhumiwa na upelelezi wa makosa ya kijinai kwa ujumla, uaandaaji wa hati za mashitaka, uhifadhi, usafirishaji na uharibuji wa vidhibiti baada ya shauri kuhitimishwa au kabla ya hapo,

Nini maana ya jinai?

Jinai ni kosa au makosa yanayofanywa na mtu au watu au taasisi kupitia watendaji wake, kinyume cha sheria au taratibu zilizoainisha makosa mbali mbali.

Je, vipi kama mtuhumiwa anataka kuandika mwenyewe maelezo yake?

Kama mtuhumiwa ameamua kuandika maelezo yake na kamtarifu afisa polisi juu ya maamuzi yake hayo, atapewa nyezo zitakazomwezesha kuandika maelezo yake kwa ufasaha.

Nini kifanyike iwapo mtuhumiwa atakaidi kutiwa nguvuni?

Kama mtuhumiwa atakaidi kutiwa nguvuni, au anatumianguvu kupinga kutiwa nguvuni, au akitaka kutoroka basi njia yeyote halali na yakufaa, kulingana na mazingira itatumika kumtia nguvuni.

Kesi ya jinai inapoanza, nani mwenye wajibu wa kutoa maelezo?

Katika kusikiliza shauri la jinai mahakamani upande wamashitaka ndio wenye wajibu wa kuanza kwa kumsomeamshitakiwa shitaka linalomkabili kama lilivyoandaliwakwenye hati ya mashitaka.

Utetezi wa haki ya kujilinda na kujihami ukoje?

Kila mtu anahaki ya kujilinda au kulinda mali yake au ya ndugu yake au rafiki yake kwa kutumia nguvu.Kwa hiyo, nguvu itakayotumika ni lazima iwe na uwianona madhara yeyote dhidi ya mtuhumiwa.

Ni mahakama zipi zinazohusika katika kutoa maamuzi ya mashauri ya jinai?

Kisheria, Mahakama Ya Mwanzo, Mahakama Ya Wilaya, Mahakama Ya Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu Na Mahakama Ya Rufaa zote zina mamlaka kutoa maamuzi juu ya mashauri ya jinai kulingana na sheria.

Kuna umuhimu gani kwa askari polisi anyefanya upelelezi kuuliza maswali na kunakili katika maandishi maelezo yanayotolewa katika upelelezi?

Kiutaratibu, mahojiano hufanyika kwa mdomo nakunakiliwa kimaandishi, na baada ya mahojiano mtoamaelezo anapaswa kutia sahihi yake kwenye maelezohayo baada ya kuridhika na usahihi wa maelezo aliyotoa. Endapo maelezo yaliyotelewa yanaendana na kutendekakwa kosa basi maelezo hayo pamoja na mtoa maelezoyatatumika katika ushahidi upande wa mashitaka pindishauri hilo litakapofikishwa mahakamani.

Utetezi wa kuchukua au Kufanya Kitendo Dhidi ya Mali Halali ukoje?

Kuchukua au kufanya kitendo au kutokufanya jambololote kwenye kitu au mali yako halali toka kwa mtumwingine aliyenayo. Kitendo hicho lazima kifanyike bila udanganyifu au ulaghai wa aina yoyote. Mfano,kutuhumiwa kwa wizi wa radio wakati ambapo radiohiyo ni mali yako.

Utetezi wa kughadhabishwa au Kukasirishwa ukoje?

Kughadhabishwa au kukasirishwa kunakotokea wakati huo huo na kupelekea kutenda kosa la jinai wakati huo huokunaweza kuwa utetezi na kinga katika makosajinai na hivyo kupelekea kutuhumiwa kutenda kosa bilakukusudia au kutokukusudia.

Mdhamini wa mtuhumiwa ana wajibu gani?

Kuhakikisha mtuhumiwa anayedhaminiwa anafanya yafuatayo; -anatimiza masharti ya dhamana na kuhudhuriamahakamani kama inavyotakiwa kufanya. -endapo mtuhumiwa atakiuka masharti ya dhamana,na hasa pale anapotoroka, itabidi mdhamini kulipakiwango cha dhamana alichojifunga. -kuwa tayari kukamatwa kwa mali zake endapomdhamini atashindwa kulipa kiwango cha fedha yadhamana. -ikiwa itashindikana kulipa kiwango cha dhamanakuwa tayari kuhukumiwa kutumikia kifungokisichopungua miezi 6 (Sita).

Nini kazi ya mahakama?

Mahakama huongozwa na hakimu au jaji pamoja nawasaidizi wake, mahakama huhusika na usikilizaji washauri na kisha kutolea maamuzi shauri lililo mbele yakekulingana na uzito wa ushahidi.

Ni chombo gani chenye mamlaka ya kumtia mtu hatiani/kumwachia hurukwa kosa la jinai?

Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kikatiba katika utawala na utoaji wa haki nchini.

Je, mahojiano baina ya polisi na mtuhumiwa yanatakiwa yanakiliwe vipi?

Mahojiano ambayo yatafanyika kwenye kituo cha polisi kati ya mtuhumiwa na afisa polisi, lazima yawekwe kwenye maandishi.

Nini lengo la mahojiano hayo?

Mahojiano hayo hufanyika kwa lengo la kukusanya taarifa zinazohusiana na uhusika wa mtuhumiwa katika tuhuma zinazomkabili.

Mfano wa makosa ya jinai ni yapi?

Mfano wa makosa ya jinai ni kama kuua, wizi, ubakaji na uhaini.

Mfumo huu unahusisha vitu gani?

Mfumo huu unajumuisha mambo mengi ikiwemo mfumo wa utendaji wa mamlaka zilizo na jukumu la kushughulika na masuala ya jinai katika nchi.

Nani mwenye mamlaka ya kutoa hati ya upekuzi?

Mkuu wa kituo cha polisi chochote ndiye mwenyemamlaka ya kutoa hati ya upekuzi ili kuruhusu zoezi laupekuzi kufanyika.

Nini kinafanyika baada ya mshtakiwa kukana kosa analoshtakiwa nalo?

Mshitakiwa akikana shitaka lililosomwa mbele yake,mahakama itanukuu maneno ya kukana shitaka nakuutaka upande wa mashitaka kuendelea na mashitakadhidi ya mshitakiwa ikiwa ni pamoja na hatua za kuitamashahidi na kutoa ushahidi kwa kadri ya mashahidi naushahidi walionao.

Nini kinafanyika baada ya mshtakiwa kukiri kosa?

Mshtakiwa akikiri kosa, hakimu atamuuliza marakadhaa kuhakikisha kauli ya kukiri kisha atanukuumaneno ya kukiri kwa mtuhumiwa katika lugha nyepesina fasaha ambayo inawakilisha kwa karibu sanayale aliyosema mtuhumiwa na kisha atamtia hatianimtuhumiwa kwa kosa alilolikiri na kisha kutoa adhabukulingana na sheria na taratibu za kimahakama.

Je, mtuhumiwa anatakiwa kuhojiwa akishakamatwa na polisi na kufikishwa kituoni?

Mtu anapokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kwa kutuhumiwa kutenda kosa la jinai, sheria inaruhusu mtu huyo kuwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa.

Utetezi wa kushitakiwa na kuachiwa Huru ukoje?

Mtu hatashitakiwa kwa kosa ambalo alishashitakiwakisha akaachiwa huru kwa kutopatikana na hatia au kwasababu nyingine ya msingi itakayotolewa na upande wamashitaka (nolle prosequi).

Utetezi wa umri mdogo ukoje?

Mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka 10 hawajibikikwa tendo lolote la jinai analotenda na anakuwa hanahatia kwenye makosa yote ya jinai. Hali kadhalika mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 yaani kumi nambili au chini yake, hatakuwa na kosa la jinai kwenyemakosa ya kujamiiana.

Je, ni nani anaweza kumkamata mtuhumiwa bila hati ya mashtaka?

Mtu yeyote anaweza kumkamata mtuhumiwa bila kuwa na hati ya ukamataji baada ya mtuhumiwa kuonekana ametenda kosa la jinai.

Utetezi wa kulazimishwa au Kushurutishwa Kutenda Kosa la jinai ukoje?

Mtu yeyote hatawajibika kwa kutenda au kuacha kutendajambo analodaiwa kutenda kisheria ikiwa amelifanyakosa husika chini ya kitisho cha kifo au kufanyiwamadhara makubwa dhidi ya maisha yake toka kwawatuhumiwa wenzake katika kosa hilo.

Nini kinafuata baada ya mtuhumiwa kufikishwa kituo cha polisi?

Mtuhimiwa akishakamatwa, akapekuliwa na taratibu za kumfikisha kituo cha polisi kukamalika, hatua inayofuata ni kumfikisha mahakamani haraka inavyowezekana.

Ni muda gani maalum uliowekwa kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa kituo cha polisi?

Mtuhumiwa anatakiwa kufikishwa mahakamani ndani ya muda wa masaa 24 kama inawezekana, au apewe dhamana kama haitawezekana kufikishwa mahakamani ndani ya muda uliwekwa na sheria, isipokuwa tu kama kosa alilotuhumiwa nalo, halina dhamana.

Mtuhumiwa anatakiwa kuhojiwa kwa muda gani?

Mtuhumiwa anatakiwa kuhojiwa akiwa kituo cha polisi kwa muda usiozidi masaa manne kuanzia alipotiwa nguvuni.

Je, mtuhumiwa anayevunja masharti ya dhamana anakuwa ametenda kosa kisheria?

Mtuhumiwa anayevunja kwa makusudi masharti yadhamana akiwa nje kwa dhamana anakuwa ametendakosa la jinai na akipatikana na hatia atawajibikakutumikia adhabu ambayo si zaidi ya adhabu ya kosaaliloshitakiwa nalo awali kabla ya kuvunja masharti yadhamana yake.

Utetezi wa mtuhumiwa kutokuwepo eneo la tukio ukoje?

Mtuhumiwa atakuwa na kinga endapo atathibitishamahakamani kwamba wakati kosa la jinai analoshitakiwalikitendeka hakuwepo kwenye eneo la tukio kwa sababuzozote zile ikiwa ni pamoja na safari au vinginevyo.

Mtuhumiwa anatiwaje nguvuni?

Mtuhumiwa atatiwa nguvuni na polisi au na mtumwingine kwa kitendo cha kumgusa bega, mkono aukwa kumzuia kuondoka kwenda sehemu anayotaka.

Utetezi wa kushitakiwa na Kuadhibiwa kwa Kosa Hilohilo ukoje?

Mtuhumiwa hatashitakiwa mara mbili baada yakutuhumiwa kwa kosa lilelile.

Ni mambo yapi ya msingi ambayo askari polisi anatakiwa kumtaarifu mtuhumiwa kabla ya mahojiano?

Mtuhumiwa kabla ya kuhojiwa anapokuwa kituo cha polisi, anapaswa kuelezwa haki zake na afisa upelelezi anayemhoji lazima amwambie jina na cheo chake, mahojiano yanapaswa kufanyika katika lugha amabayo mtuhumiwa anaielewa vyema na pia mtuhumiwa asihojiwe mpaka awe amepewa tahadhari kwamba, hawajibiki kujibu maswali atakayoulizwa na afisa wa polisi mpelelezi na pia anayo haki ya kuwasiliana na mwanansheria wake ili awepo katika mahojiano hayo.

Je, katika ombi hilo, mahakama inampatia mtuhumiwa haki ya kusikilizwa?

Mtuhumiwa, kupitia mahakama baada ya maombi hayo kupelekwa na afisa upelelezi, atapewa haki ya kusikilizwa yeye mwenye au kupitia mwanansheria ambaye atamwakilisha katika maombi hayo ya kuongeza muda wa kuhojiwa dhidi yake.

Je, askari polisi anaweza kukataa kutoa dhamana?

Ndio na kama itatokea askari polisi kukataa kutoa dhamana kwamtuhumiwa basi watatoa sababu za kukataa kimaandishi.

Je, ni lazima kwa askari polisi kujitambulisha?

Ndio, askari polisi au mtu yeyoteanayekamata anatakiwa ajitambulishe kwa mtuhumiwa kwa kutaja Jina lake, hata kituo anachofanyia kazi nakutoa kitambulisho cha kazi.

Je, askari polisi anaweza kutoa dhamana?

Ndio, askari polisi wanayo mamlaka kutoa dhamana kwamtuhumiwa kuwa nje ya kizuizi.

Je, askari polisi ana wajibu wa kumpa mtuhumiwa taarifa mtuhumiwa juu ya kuongezwa kwa muda wa mahojiano?

Ndio, ikiwa muda wa mahojiano utaongezwa kuzidi masaa manne ya msingi yaliyowekwa na sheria, mtuhumiwa anayo haki ya kujulishwa juu ya kuongezwa kwa muda huo wa mahojiano kati yake na afisa upelelezi akiwa chini ya uangalizi wa polisi.

Je, dhamana ya mahakama inatolewa kwa mtuhumiwa yeyote?

Ndio, inaweza kutolewa kwa mtuhumiwa yeyote isipokuwa yule aliyetuhumiwa kufanya makosa yafuatayo; -Mauaji -Uhaini -Wizi wa kutumia silaha kubwa za moto -Kufanya biashara ya madawa ya kulevya ambayoyametajwa katika sheria ya Kuzuia Madawa ya Kulevya.

Je, kuna kinga yeyote au utetezi wowote dhidi ya makosa ya jinai?

Ndio, kisheria zipo kinga mbalimbali ambazo mtuhumiwa anaweza kuzitumia.

Je, mahakama kuu ina mamlaka ya kubadili masharti yaliyowekwa na mahakama za chini?

Ndio, mahakama kuu ina mamlaka ya kubadilisha masharti ya dhamana ambayo yamewekwa na mahakamaza chini na kumpa dhamana mtuhumiwa ambayeatakuwa amekataliwa dhamana na mahakama za chini.

Je, muda huo unaweza kuongezwa? Na kama ndio, nani anaweza kuongeza muda huo?

Ndio, muda wa mahojiano unaweza kuongezwa kwa kipindi kisichozidi masaa manane ikiwa afisa wa polisi (mfawidhi) anayepeleleza tukio au tuhuma zinazomkabili mtuhumiwa anayehojiwa kwa wakati huo ataona inafaa kufanya hivyo.

Ni ofisi gani ya serikali ambayo inahusika moja kwa moja katika kuendesha kesi za jinai?

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali.

Je, ni pande ngapi zinahusika katika kusikiliza kesi ya jinai?

Pande hizo ni; -Mahakama -Mashitaka -Utetezi wa Mashitaka

Polisi anatakiwa kuuliza maswali ya aina gani kwa mtuhumiwa?

Polisi anaruhusiwa kumuuliza mtuhumiwa maswali yoyote wakati wa mahojiano hayo kwa lengo la kupata taarifa muhimu kuhusu kosa alilotuhumiwa nalo.

Nini maana ya upekuzi na nani anatoa mamlaka ya kufanya upekuzi?

Sheria inampa askari polisi mamlaka ya kufanya upekuzi katikanyumba za kuishi watu, ofisi, magari, vyombo vyovyoteau maeneo yeyote kama atakuwa na sababu za msingikufanya hivyo. Upekuzi pia unaweza kufanywa kwa mtu yaani katika mavazi yake au vitu alivyobeba.

Je, askari polisi anaweza kumkataza mtuhumiwa kuwasiliana na ndugu/mwenza/mwanasheria wake?

Sheria inampa haki polisi mpelelezi anayemhoji mtuhumiwa, kumzuia mtuhumiwa kuwasiliana na mwanasheria wake au ndugu zake, kama anaamini kwamba mawasiliano hayo yanalenga kusaidia kutoroka kwa mtuhumiwa mwenza, endapo tuhuma zinamhusu mtuhumiwa zaidi ya mmoja au ikiwa mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kupotea au kuharibiwa kwa ushahidi wowote ambao unaweza kujumuishwa katika shitaka dhidi ya mtuhumiwa anayehojiwa.

Askari polisi atafanya nini pale ambapo anahitaji muda wa ziada wa kumuhoji mtuhumiwa kama muda wa nyongeza umeisha?

Sheria inamruhusu afisa upelelezi kupeleka maombi mahakamani ya kuongeza zaidi muda wa mahojiano kabla ya muda wa msingi wa masaa manne kuisha au baada ya muda wa nyongeza wa masaa nane kuisha.

Ni makosa yapi ya jinai yanaenda mahakama ipi?

Sheria mbalimbali zimeainisha makosa mbalimbali na mahakama zenye mamlaka ya kusikiliza na kutolea maamuzi mashauri yao. Kwa mfano, mashtaka ya mauaji na uhaini yanasikilizwa na kutolewa maamuzi na Mahakama Kuu pekee.

Je, ni sheria ipi inayosimamia makosa ya jinai kwa kiasi kikubwa?

Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 ya sheria za Tanzania (the Penal Code). Japo, kuna sheria nyingine mbalimbali zinazosimamia pia makosa ya jinai.

Ni sababu ipi inazotumiwa na upande wa mahstaka katika kuomba mtuhumiwa asipunguziwe adhabu?

Tabia ya mtuhumiwa kurudia rudia kosa husika ambalo ni kero katika jamii na kuwa kama fundisho kwawengine.

Ni sheria ipi inayoelezea taratibu zote za kukamatwa hadi kuendeshwa kwa mashauri ya jinai?

Taratibu za kukamata hadi kuendesha mashitaka ya jinai husimamiwa na Sheria ya Mwenendo wa Makosa yaJinai ya Mwaka 1985 (Sura ya 20) na sheria nyinginekulingana na kosa la jinai.

Je, nini tofauti kati ya makosa ya jinai na makosa ya madai?

Tofauti kati ya Jinai na madai ni kwamba, kosa la jinai huhesabiwa ni kosa dhidi ya Jamhuri na madai ni lalamiko dhidi ya mtu binafsi, kampuni, taasisi au serikali kutokana na makubaliano fulani.

Nini kazi ya upande wa utetezi?

Upande huu unahusisha mtuhumiwa na mashahidi wakeambao watamsaidia katika utetezi wake kwa kukanushamashitaka dhidi yake. Kazi ya utetezi inaweza kufanywa na mtuhumiwa mwenyewe au wakili wake atakayempatakutoka kwa mawakili binafsi.

Nini kazi ya upande wa mashtaka?

Upande wa mashitaka ni Jamhuri, yaani Serikalina vyombo vyake ambavyo ni pamoja na Polisi,TAKUKURU, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Ofisiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au taasisi yoyoteyenye mamlaka ya kuendesha mashitaka, mwathirika wakosa la jinai, pamoja na mashahidi watakaounga mkonomashitaka.

Nini hasa ni dhumuni la upelelezi?

Upelelezi katika utawala wa haki jinai husaidia katika kutambua ni kosa gani hasa la jinai liliotendeka, kuwabaini wahusaika, kubaini shitaka lipo kwa mujibu wa sheria gani na mwisho ni kutambua mahakama sahihi yenye uwezo na mamlaka kisheria kusikiliza shitaka linalokusudiwa.

Nani anapaswa kufanya upelelezi wa makosa ya jinai?

Upelelezi wa makosa ya jinai hufanywa na jeshi la polisikupitia askari maalumu wenye utalaamu wa kufanya kazihiyo.

Je, nini maana ya utawala wa haki jinai?

Utawala wa haki jinaini mfumo wa usimamizi na utekelezaji wa sheria za nchi zinazohusu mwenendo wa makosa ya jinai.

Subscribe to Our News Letter

Subscribe to our newsletter to get the latest news and updates from Sheria Kiganjani

logo

Various Topics

  • The Beginning
  • Topic
  • About
  • Communicate with us
  • Article
  • Landesa

Working Hours

  • Monday - Friday
  • 08:00AM - 5:00PM
  • Saturday
  • 08:00 - 1:00PM

Call us: +255 621 900 555

Email: [email protected]

Visit us

7th Floor, Tanzanite Park Victoria Area POBOX 6622 Dar Es Salaam

Copyright © 2025 All Right Reserved Law in the palm of your hand